Lengo kuu ya jumuiya yetu ni kumtangaza Bwana YESU aliye alfa na omega katika historia ya wokovu wa binadamu wote hapa duniani.
Pages
- Home
- MALENGO YA JUMUIYA
- NGUVU YA ROZARI TAKATIFU
- PICHA ZA BWANA YESU
- AMRI ZA MUNGU
- AMRI ZA KANISA
- MFUMO WA UONGOZI
- SALA YA ASUBUHI
- SALA YA JIONI
- SALA MBALI MBALI
- MASOMO YA JUMAPILI NA TAFAKARI
- UMUHIMU WA SKAPULARI
- MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU
- KATEKISIMU KATOLIKI
- UFASIRI WA BIBLIA KATIKA KANISA
- “ROZARI YA BIKIRA MARIA”
- NANI MWABUDU SANAMU ?
- CONTACT US
- PICHA ZA BIKIRA MARIA
- HISTORIA NA UKUU WA BIKIRA MARIA
Monday, February 3, 2014
Mheshimiwa Padre Vincent Mduduzi Zungu ateuliwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Port Elizabeth, Afrika ya Kusini
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Vincent Mduduzi Zungu, kutoka Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Port Elizabeth, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu Askofu mteule alikuwa ni msimamizi Wakapuchini kutoka Kusini mwa Afrika, kwenye Makao Makuu ya Shirika mjini Roma.
Askofu mteule Vincent Mduduzi Zungu alizaliwa tarehe 28 Aprili 1966, Jimboni Eshowe. Baada ya majiundo na malezi ya Kipadre na kitawa, akaweka nadhiri zake za daima hapo tarehe 2 Julai 1994 na kupewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 8 Julai 1995.
Baada ya Upadrisho alitekeleza utume wake kama Paroko msaidizi, Mlezi wa Wanovisi, Jalim na baadaye alichaguliwa kuwa ni Padre Mkuu wa Kanda ya Wakapuchini Afrika ya Kusini.
Itakumbukwa kwamba, tangu Mwaka 2011 Jimbo la Port Elizabeth lilikuwa wazi baada ya Askofu Michael Gower Coleman kung'atuka kutoka madarakani kwa sababu za kiafya.
Habari :radio vaticana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment