Wednesday, June 4, 2014

Acheni bifu tujenge nchi!

  

Rais Arthur Peter Mutharika wa Malawi baada ya kuapishwa anataka kuanza kuandika ukurasa mpya wa Malawi kuhusiana na sera ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa sanjari na kupambana na rushwa pamoja na ufisadi uliokithiri nchini Malawi.


Huu ndio mwelekeo unaooneshwa na Rais Mutharika baada ya kuapishwa kuwa Rais Mpya wa Malawi baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Malawi hapo tarehe 20 Mei 2014. Ni matumaini ya Rais Mutharika kwamba, viongozi wa vyama vya kisiasa nchini Malawi watazika tofauti zao na kushikamana kwa ajili ya ujenzi wa Malawi mpya inayosimikwa katika haki, demokrasia na maendeleo ya kweli!


Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mutharika zilihudhuriwa na wajumbe wengi kutoka ndani na nje ya Malawi, lakini ni Rais Seretse Khana Ian Khama wa Botswana ndiye alihudhuria kama mkuu wa Nchi, jambo ambalo limewashangaza wengi. Malawi inataka kuanzisha urafiki na nchi zinazoibukia katika uchumi kimataifa kama vile Brazil, China, India na Afrika ya Kusini.


Habari kwa hisani ya radio vatican


No comments:

Post a Comment