Wataalam
katika sekta ya afya wanasema kwamba, ugonjwa wa Ebola unaendelea
kupukutisha maisha ya watu wengi Afrika Magharibi, kiasi kwamba, kwa
sasa kunahitajika rasilimali watu na fedha ili kukabiliana na mlipiko wa
ugonjwa huu. Kwa mara ya kwanza ugonjwa wa Ebola umejitokeza huko
Afrika ya Magharibi hasa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Ugonjwa huu unaendelea kuenea zaidi kutokana na wananchi wengi kutozingatia mashariki yaliyowekwa. Watu wanashiriki mazishi hata kwa watu waliofariki dunia kwa ugonjwa wa Ebola jambo ambalo ni hatari na limeendea kuwa ni chanzo cha kuenea kwa ugonjwa huu huko Afrika Magharibi. Zaidi ya watu 500 wamekwisha ambukizwa virusi vya Ebola na zaidi ya watu 300 tayari wamekwisha fariki dunia. Hapa kuna haja ya kupata madaktari walioandaliwa ili kusaidia kuwaelimisha na kuwatibu watu wanaopambana na ugonjwa wa Ebola, lakini pia vinahitajika vifaa tiba na dawa ili kutokomeza ugonjwa wa Ebola.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment