Friday, June 13, 2014

Rais Danilo Sànchez akutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Juni 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Danilo Medina Sànchez kutoka Jamhuri ya Watu wa Domenican ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wamepongeza uhusiano mwema uliopo kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa Domenican, lakini zaidi ni kutokana na mchango wa Kanisa Katoliki nchini humo katika ustawi na maendeleo ya wananchi wote katika sekta ya elimu, afya na maendeleo endelevu. baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake wamegusia pia masuala muhimu ya kikanda na kimataifa hasa kuhusiano na tatizo la wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya kisiasa bila mafanikio!

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment