Yesu
anatufundisha vigezo vitatu katika kuishinda misuguano kati yetu,
kwamba ni ; uhalisi, uthabiti na mapenzi ya dhati, ni malezo ya Papa
Francisko , Alhamisi asubuhi, katika maadhimisho ya Ibada ya Misa
aliyoiongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, akilenga katika
upendo wa kidugu, ambao Yesu alifundisha wanafunzi wake.
Katika mahubiri yake, Papa Francisko aliangalisha katika somo la Injili ambamo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “ iwapo haki yao haitazidi haki ya waandishi na Mafarisayo , kamwe hawataigia katika ufalme wa Mbinguni. " Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa msiue; na mtu akiua itampasa huku, bali mimi ninawaambieni kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu na mtu akimfyolea ndugu yake itampasa baraza na mtu akimwapiza nduguye itampasa jehanam( Mt 5: 20-21)".
Papa alihoji iwapo upendo kati yetu, unalingana na mafundisho ya Yesu? Alisema, Yesu anatuambia kwamba sisi lazima kumpenda jirani yetu, na kuwa tofauti na Mafarisayo ambao waliyajua vyema maandiko lakini hawakuwa thabiti katika kuyazingatia mafundisho, walimezwa na vivuli vingi vya itikadi, bila ubinadamu. Papa alifafanua uzingatiaji wa sheria na kanuni bila ubinadamu, ndani mwake mnapungukiwa na upendo wa kweli, ni kutompenda jirani.
Papa anaendelea kueleza, vigezo vitatu vilivyotolewa na Yesu katika somo hili kwamba, kwanza ni uhalisia. Alifafanua , vigumu sana kujirekebisha iwapo kuna kinyongo dhidi ya mwingine, kwanza ni kutafuta ufumbuzi wa kuondoa kinyongo hicho . Ni lakini lazima kuridhiana, na kutembea pamoja katika njia ya maisha kwa kupendana licha ya kila mmoja kuwa na namna zake za kufikiri. Ni jambo jema kupatana.
Papa aliongeza , nguvu ya kuwa na makubaliano, ambamo kila mmoja anabaki na imani yake, hubaki kuwa nyeti na mara nyingi haipendezi. Lakini inapaswa kuridhiana kwa ajili ya kuokoa mambo mengi, ni lazima kuwa na makubaliano, ambamo kila mmoja atachukua hatua kwa mujibu wa imani yake lakini kwa mtazamo wa kudumisha amani. Amani ya kudumu ni muhimu sana. Yesu, aliongeza, "pia anasema, tuwe na uwezo wa kufanya kuridhiana kati yetu, mikataba inayozidi ile ya haki ya Mafarisayo na walimu wa sheria. Kuna hali nyingi za binadamu, aliongeza, wakati wa kutembea pamoja katika hija ya maisha ya hapa duniani. Hivyo ni kusafiri pamoja kwa kuvumiliana, na kuacha chuki na vita kati yetu.
Papa alieleza kigezo cha pili anachotupa Yesu, ni kigezo cha kuwa Wakweli. Hapa ameonya dhidi ya udaku kwamba, ni kuua mengine, kwa sababu uongo na uzushi ni mzizi wa chuki. Chuki huua katika njia tofauti. Uzushi na matusi, ni kashfa, Yesu anaonya. Aliendelea leo hii wengi ni hudhani , udaku, uzushi , na matusi hayana madhara , lakini madhara yake ni makubwa , kiasi kwamba huua, kwa kuwa hujenga chuki na fitina kati ya watu. Matusi yenye kuwa na asili moja ya uhalifu ni sawa na chuki. Papa alieleza na kutoa wito kwa watu wote kujiepusha na roho hii ya uongo, udaku na uzabina, badala yake wadumishe kweli, hata wakati wa porojo.
Papa alitaja kigezo tatu kilichotolewa na Yesu kuwa ni upendo wa dhati unaotushikamanisha kama ndugu wa Baba Mmoja. Hivyo, kitendo chochote cha kumdhuru binadamu mwingine ni dhambi. Papa alieleza na kuasa wale wenye kusema siwezi kwenda kwa Baba kwa sababu, sina amani na ndugu yangu. Vivyo hivyo huwezi kuzungumza na Baba kama huna amani na ndugu yako. Hivyo ni jambo jema kukubaliana na ndugu yako kabla ya kuamua kwenda kwa Baba. Hiki ni kigezo cha tatu ambamo Yesu anatuambia sisi sote tu wana wa Baba mmoja, kigezo cha udugu katika “uwana” , na hivyo hatupaswi kuua au kutukana wengine kwa kuwa matusi huua. Yesu anatutaka tuondokane na unafiki wa haki ya waandishi na Mafarisayo. Papa anakiri jambo hili si jepesi, lakini ndiyo njia ambayo Yesu anatuambia tuendelee kutembea nayo.
Papa alimalizia kwa kuomba neema ya kusonga mbele kwa amani kati yetu , tena kwa makubaliano na mshikamano katika roho ya kuwa wana wa Baba mmoja, roho ya “uwana. "

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment