Friday, July 11, 2014

Msiogope kujiachilia mikononi mwa Mungu!


Athari za myumbo wa uchumi kimataifa, vita, kinzani na migogoro bila kusahau magonjwa na majanga mbali mbali yanayoendelea kumwandama mwanadamu katika maisha yake. Yote haya ni mambo yanayochangia kwa watu wengi kukata tamaa ya maisha na hivyo kujiona kuwa si mali kitu na kwamba, kwao maisha hayana tena dira wala mwelekeo!

Katika mazingira kama haya, watu wanapata "kigugumizi" cha kufanya maamuzi magumu katika maisha yao: kwa mfano vijana kufunga ndoa na kuanza maisha ya unyumba kwa kutambua kwamba, ndoa kati ya Bwana na Bibi kadiri ya Mpango wa Mungu katika maisha ya mwanadamu ni zawadi ya kudumu! hali kama hii inaweza kuwakuta hata vijana wanaotaka kujiunga na maisha na wito wa Kipadre na Kitawa!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawahamiza waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujiachilia mikononi mwa Mwenyezi Mungu: wawe tayari kutekeleza wito na mwaliko wake, kwani kwa lolote analowataka kulifanya atawakirimia maradufu!

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment