Baba
Mtakatifu Francisco akikutana na waandishi wa habari akiwa ndani ya
ndege tokea Korea, alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mazungumzo na
Serikali ya China, alijibu kwamba, kwanza kabisa, anaweka mkazo katika
sala ya kuombea viongozi wanaohusika katika majadiliano hayo wajaliwa
hekima na busara. Na aliyapeleka mawazo yake kwa Padre Mjesuiti Matteo
Ricci, aliyeonyesha upendo mkuu kwa watu wa China. Na pia kama Papa
Mstaafu Benedikto XVI alivyoandika katika barua yake kuhusu mahusiano
na China, barua hiyo bado ni muhimu, na inafaa kusomwa tena na tena.
“Kiti Kitakatifu”, alisema, “daima ni wazi katika kuwasiliana”, kwa
sababu kina heshima ya kweli kwa watu wa China".
Papa pia alizungumzia ziara yake ijayo katika taifa la Albania, akisema, haendi huko, kujifurahisha kama baadhi wanavyoweza kuhisi, lakini kwa sababu anapenda kuanza kuyatembelea mataifa yaliyo baki pembezoni. Alitaja sababu mbili za kwenda Albania kwanza, kwa sababu serikali ina umoja wa kitaifa, ambayo huunganisha Waislamu, Orthodox na Wakatoliki, shukrani kwa Baraza linalounganisha wajumbe kutoka dini mbalimbali, na matunda ya kazi yake inaonekana katika mizani. Na hili ni jambo jema, kutangaza wengine kwamba, inawezekana kufanya kazi kwa pamoja!" Sababu ya pili alisema, inahusu historia ya Albania, ambayo ilikuwa ya kipekee miongoni mwa mataifa kikomunisti ambayo yalikuwa na Katiba ya Ukana Mungu vitendo. Kwenda Kanisa ilikuwa ni kutenda kinyume cha katiba! Na pia alikumbuka kwamba 1820, makanisa yaliharibiwa katika taifa hilo la Albania. Na hivyo leo hii, kukiwa na mabadiliko makubwa ya kisasa ni vyema kwenda huko kuimarisha roho hii ya umoja na mshikamano wa kitaifa licha ya tofauti za imani.
Aidha alieleza nia yake ya kutembelea Philadelphia mwaka ujao kwa ajili ya Mkutano wa Familia ya Dunia na akisema, pengine itakuwa ni kujibu wingi wa mialiko iliyotoka sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na New York, Mexico na Hispania. Lakini, safari hiyo bado haijatolewa maamuzi.
Na akijibu swali juu ya uhusiano wake na Papa Mstaafu Benedict XVI, Papa Francisco alisema alitembelea yake kabla ya kuanza safari ya kutembelea Korea na walijadili maswali ya kitheolojia. Na kwamba, anaona kujiuzuru kwake ilikuwa ni wito katika unyenyekevu na ishara ya ujasiri. Na iwapo hali itakuwa pia hivyo kwake , atafikiria kufanya vivyo hivyo. Benedikto XVI, amefungua mlango mwingine wa taasisi na si jambo la kipekee.
Na pia alijibu swali iwapo ana mpango wa kutembelea Japani kwa ajili ya kuombea Wakristo walioteseka kama ilivyo Korea. Alisema, ndiyo, tayari amekwisha pata mwaliko kutoka serikali ya Japan na Maaskofu na kwamba, atafurahi kufanya hivyo. Na alizungumzia mateso ya kihistoria ya Korea na mgawanyiko uliounda mataifa mawili akisema, pamoja na mgawanyiko huo watu wa Korea hawajapoteza utu wao. Watu hawa walivamiwa na unyonge wa mateso na vita, na hadi sasa wanaendelea kuteswa na utengano. Na kwa kifupi alifany arejea katika Ibada ya Misa aliyoiongoza siku ya Jumatatu ya Misa mjini Seoul, kama sehemu ya kuwafariji wanawake wakongwe waliodhulumiwa kingono na jeshi la Japan, wakati wa vita Kuu ya II na ambao wamekuwa wakitafuta kuombwa msamaha rasmi na serikali. Papa Francisco alikemea unyama huo, na kuwafariji kwamba bado hawajapoteza heshima ya utu wao.
Aliendelea kusema , hata leo hii dunia iko katika mapambano ya vita vinavyo sikika kila mahali. Papa Francis kisha alirejea maoni yaliyotolewa siku za nyuma kwake kwamba , duni aiko ktika Vita kuu ya Tatu. Dunia iko katika vita na madhulumu ya ukatili wake unafanyika kila mahali. Papa alikamilisha barizi na wanahabari akisema, mara atakapo rejea Roma, atakwenda katika Kanisa la Bikira Maria Mkuu kutoa shukurani zake kwa majaliwa ya safari njema.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment