Wednesday, August 20, 2014

Wafuasi wa Papa Francisko kwenye mtandao kwa sasa wamevuka millioni 15


Baba Mtakatifu Francisko tangu kuchaguliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki ameendelea kutumia mitandao ya kijamii kama njia ya kuwasiliana na watu moja kwa moja. Mtandao wa twitter ya Baba Mtakatifu, ulifunguliwa na Papa mstaafu Benedikto XVI kunako Desemba 2012. Takwimu zinaonesha kwamba, hadi sasa wafuasi wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye mtandao wake wa twitter wamevuka millioni 15.

Wafuasi wa Baba Mtakatifu katika lugha ya Kihispania wanaongoza kwa idadi ya watu 6, 479, 550. Wanafuata watumiaji wa lugha ya Kiingereza ambao idadi yao kwa sasa imefikia wafuasi 4, 366, 300. Wafuasi wanaotumia lugha ya Kiitalia ni 1, 867, 400. Wafuasi wanaotumia lugha ya Kireno ni 1, 123, 800; watumiaji wa lugha ya Kifaransa ni 291, 800; wanaotumia lugha ya Kilatini ni 271, 600; Kipolandi ni 251, 100 na Kiarabu wamefikia wafuasi 145, 500.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment