Monday, March 26, 2012

JUMUIYA MPYA IMEANZAISHWA !

MSALABA WA MKOMBOZI WETU YESU KRISTU
Wapendwa TUMSIFU YESU KRISTU !. Kwa upendo wa Mungu imeanzishwa jumuiya mpya ya BIKIRA MARIA MALKIA WA MALAIKA katika parokia ya mpya ya Kongowe, hivyo tunawakaribisha wote katika jumuiya yetu ili tumwabudu Mungu pamoja katika sala.

Hiki ni kipindi cha Kwaresma ambapo tunakumbuka jinsi mkombozi wetu Bwana YESU KRISTU alivyoteseka ili kutukomboa watu wote kutoka dhambini hivyo tunaalikwa wote kufunga na kufanya matendo ya huruma kwa watu wenye shida mbalimbali kama wagonjwa, maskini, watoto yatima na makundi mengineyo ambayo yanahitaji misaada mbalmbali.

Asanteni

AMANI NA SALAMA

No comments:

Post a Comment