IJUMAA KUU KATIKA PICHA
HUU NDIO MSALABA AMBAO MWILI WA
BWANA ULITUNDIKWA, WOTE
TUUABUDU DAIMA.
MSALABA NI ISHARA KUU YA UKOMBOZI
WETU WOTE TUUABUDU!
ANGALIA BWANA YESU ALIVYOTESEKA
YOTE HAYA NI KWA AJILI YA UPENDO
WAKE KWETU,JAMANI TWENDENI KWAKE
ATUPE AMANI NA HATUTA KUWA WAONGO
NA WANAIKI, HATUTA JILIMBIKIZIA MALI
KWA MANUFAA YA WACHACHE, HATUTA
GEUZA MALI ZA UMMA KUWA ZA WATU BINAFSI.
ANGALIA ASKARI HAWA WOTE WANATAKA
KUMSULUBISHA MKOMBOZI WETU, JE SISI
HUMSULUBISHA MKOMBOZI MARA NGAPI?
ASANTE YESU KWA MSALABA WAKO MTAKATIFU!
E BWANA YESU NISAMEHE DHAMBI ZANGU
KWA KUWA NAKUPENDA WEWE
DAIMA.
BWANA ASULUBIWA KATI YA
WANYANGANYI ILI SISI SOTE
TUOKOLEWE.
MSALABA MZITO, KWELI BWANA ULITESEKA
SANA NAOMBA KUPITIA MATESO YAKO
NIPONYE MWILI NA ROHO YANGU.
MAMA MARIA UTUOMBEE SASA
NA SAA YA KUFA KWETU.
MAMA YETU KWELI ALIPATA
MAUMIVU MAKALI KWA AJILI YA
UKOMBOZI WETU.
No comments:
Post a Comment