KWA KUWA UMEWAKOMBOA WATU KWA MSALABA WAKO MTAKATIFU !
Ndugu mpendwa TUMSIFU YESU KRISTU !
Hakika bwana amepata mateso makubwa kwa ajili ya ukombozi wetu sisi sote tuliopo katika dunia hii, na hii ni kutokana na upendo wake uliotukuka kwetu, kweli mkombozi ni njia yetu na mwanga wetu. Basi yatupasa kufanya matendo yaliyo mema ya kumtukuza Mungu ili tuweze kuishi vyema kama bwana alivyotufundisha.
Yatupasa kufanya nini katika Taifa letu la Tanzania na Dunia kwa Ujumla.
- Kuacha kuwadhulumu wengine hasa walio maskini.
- Kuacha mara moja kutumia nafasi zetu kujinufaisha.
- Kuacha kutumia rasilimali za nchi kwa ajili ya wachache.
- Tuzishike na kuzifuata AMRI ZA MUNGU.
- Tuhakikishe tunaifanyia kazi AMRI KUU YA UPENDO.
- Viongozi wa selikali waache ubinafsi.
- Kwenye familia zetu tuache ubinafsi na tusali pamoja.
- Tuseme hapana kwenye mambo yote yanayokwenda kinyume na mpango wa MUNGU.
- Katika kipindi cha kwaresma tutubu dhambi zetu na kujiweka karibu na mkombozi ili kuchota neema zake.
- Tuwaombee viongozi wetu wa nchi na wa dini watekeleze majukumu yao isapavyo.
AMANI NA SALAMA !
No comments:
Post a Comment