Baba
Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu,
Alhamisi kuu jioni, tarehe 17 Aprili 2014, kwenye Jumuiya ya Mfuko wa
Don Gnochi, iliyoko mjini Roma. Siku ya Alhamisi kuu jioni, Mama Kanisa
anaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kama sehemu ya kumbu kumbu endelevu
ya Siku ile Yesu alipoweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu sanjari na
Sakramenti ya Daraja Takatifu, zinazomwilishwa katika huduma ya upendo
hasa kwa watu wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.
Jumuiya hii inawahudumia watu wenye matatizo ya afya wanaohitaji msaada wa pekee ili kuweza kurudia tena katika hali yao ya kawaida na kuingizwa tena katika maisha ya kijamii. Kimsingi ni watu wenye ulemavu, ambao wanapewa huduma kwenye Jumuiya hii ya Don Gnochi. Katika Ibada hiyo itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, wagonjwa, jamaa, wafanyakazi na uongozi wa kituoni hapo watashiriki.

taarifa kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment