Thursday, May 29, 2014

Papa ataja nia ya Hija yake katika nchi Takatifu


Kama kawaida ya kila Jumatano , Papa akiwa Vatican , alitoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Katika Katekesi hii , ametaja hasa nia za kufanya hija katika Nchi Takatifu , aliyokamilisha siku ya Jumatatu, akieleza kwamba, hija hii imekuwa ni zawadi kubwa kwa Kanisa, na hivyo anamtolea Mungu shukurani. Kwa majaliwa ya Mungu, aliweza kuitembelea nchi hii iliyobarikiwa , yenye kuwa na matukio ya kihistoria ya Ukombozi ulioletwa na Yesu, matukio msingi kwa Wayahudi, Wakristo , na Waislamu.
Aidha Papa kwa mara ingine ametoa shukrani zake za dhati kwa Mwenye Heri Patriaki Fouad Twal , Maaskofu wa madhehebu mbalimbali, Mapadre, na Wafranciskani wenye kazi ya ulinzi katika Maeneo Matakatifu. Shukrani zake pia amezitoa kwa Wakuu wa Nchi wa Jordan , Israel na Palestina, kwa wema fadhila na mapokezi mazuri waliyompatia , yeye mwenyewe pamoja na wale wote alioandamana nao katika ziara hii.

Baba Mtakatifu ametaja malengo makuu ya ziara hii kuwa matatu, kwanza ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa kihistoria kati ya Papa Paulo VI na Patriaki Athenagoras . Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Mrithi wa Petro, kutembelea Nchi Takatifu . Ziara iliyo weka alama msingi katika njia ya kutembea pamoja kuelekea umoja kamili wa Wakristu. Katika ishara hii ya kinabii, Askofu wa Roma na Patriaki wa Constantinople kwa Pamoja, walitolea sala zao katika kaburi la Yesu, wakiwa pia na Viongozi wengine wa Makanisa mbalimbali na jamii, mamlaka ya kiraia na waamini wengi. Mahali hapo ambapo kunatoa mwangwi mpya unao tangaza Ufufuko wa Kristo , waliweza kuyasikia upya uchungu wote na mateso ya mgawanyiko kwamba bado upo kati ya wafuasi wa Kristo.Lakini juu ya yote , katika mwitikio wa jibu linalo dai kuheshimiana kwa udugu na upendo, unaohimizwa na sauti ya kubwa ya Mchungaji Mwema Mfufuka na peke , anayetaka wafuasi wake wawe kundi mmoja . Na hivyo walipata hisia kali katika haja ya kuponya majeraha ambayo bado yanaumiza na kuwa thabiti katika njia ya kuelekea ushirika kamili .

Papa Francisko pia ametaja nia ya pili ya Hija yake , kwamba ilikuwa ni kuhimiza wale wote wanaohusika na kazi ya kufanikisha amani kaika eneo la Mkoa wa Mashariki ya kati na wale wote wanaotoa huduma za ubinadamu kwa watu wateswa hasa wakimbizi, watoto , wazee na watu wengine dhaifu katika jamii, kutenda kwa bidii zaidi kufanikisha amani na utulivu. Alikwenda kama Nabii wa Kitume, kuhimiza uwepo wa nyoyo za huruma, kwa ajili ya watoto ya dunia hii ambayo kwa muda mrefu, imeishi na vita, wawe tena na haki ya kukamilisha siku ya mwisho kwa amani ! Kwa nia hiyo, Papa ametoa wito kwa Wakristo kuondoa uchungu kwakuwa moyo wazi na utulivu unao jazwa na Roho Mtakatifu, kwa kuwa, uwezo wa ishara ya unyenyekevu , udugu na maridhiano, huweza kuhamisha milima ya uchungu. Na hilo linawezekana kwa kuchukua tabia hiii ya unyenyekevu na maridhiano katika maisha ya kila siku , kukubali kuishi na watu wa tamaduni na dini mbalimbali , na hivyo kuwa mafundi wa amani. Papa alieleza kwa kukumbuka migogoro ya Syria Israel na Palestina.
Papa ametaja nia yake ya tatu kuhiji katika Nchi Takatifu kwamba pia ilikuwa ni fursa ya kuthibitisha imani kwa jamii ya Kikristo, ambao inakabiliwa na changamoto nyingi . Na pia kutoa shukrani za Kanisa zima kwa uwepo wa Wakristo katika eneo hilo na katika Mashariki ya Kati . Hawa ndugu ni mashahidi ujasiri wa matumaini na mapendo, " chumvi na mwanga" katika nchi hiyo. Kwa maisha yao ya imani na sala , na kukubaliwa kwa shughuli za elimu na hisani, katika neema ya maridhiano na msamaha , huchangia manufaa ya jamii.

Pamoja na Hija hii, ambayo ilikuwa neema ya kweli ya Bwana, Papa alipenda kutoa neno la matumaini kwao wote na kwake pia aliweza kupokea mengi kutoka ndugu zake wake kwa waume wenye kuwa na matumaini, kwa njia ya mateso mengi , kama vile wale ambao walikimbia nchi yao kwa sababu ya mapigano; kama wale wa wengi katika sehemu mbalimbali za dunia , ni kudharauliwa na kubaguliwa kwa sababu ya imani yao katika Kristo. Sisi kuendelea kukaa karibu nao ! Tunaomba kwa ajili yao na kwa amani katika Nchi Takatifu na katika Mashariki ya Kati . Maombi ya Kanisa zima pia husaidia njia ya kuelekea umoja kamili miongoni mwa Wakristo, ili ulimwengu upate kuamini katika upendo wa Mungu katika Yesu Kristo amekuja kukaa miongoni mwetu.

No comments:

Post a Comment