Friday, June 13, 2014

Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuundwa Sudan ya Kusini katika kipindi cha miezi miwili!


Serikali ya Sudan ya Kusini pamoja na waasi wamefikia makubaliano ya kusitisha vita kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa, kama njia ya kukata mzizi wa fitina, chuki na uhasama uliojitokeza nchini humo mwezi Desemba 2013.

Makubaliano haya yamefikiwa kati ya Rais Salva Kiir Mayardit na Bwana Rijek Machar, kiongozi wa kundi la waasi nchini Sudan. Makubaliano haya ni juhudi za IGAD kutaka kuleta amani, utulivu na maendeleo katika eneo hili ambalo limekuwa uwanja wa fujo kwa miaka ya hivi karibuni!

Waziri mkuu wa Ethiopia amewaonya wahusika wakuu wa pande hizi mbili kuhakikisha kwamba, wanaheshimu na kutekeleza kwa dhati makubaliano yaliyofikiwa, vinginevyo, watachukuliwa hatua kazi ikiwa ni pamoja na kuwekewa vizuizi kwa wale watakaobainika kuhusika na uvunjwaji wa mkataba huo!

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment