Sunday, June 1, 2014

Wakristo Palestina watakiwa kutouza ardhi yao


Mwaliko umetolewa kuwaalika Wakristo ,kutoihama kutoka Nchi Takatifu. Ni wito wa Patriaki wa Antokia ya Wamaronaiti , Patriaki Bechara Boutros Rai , ambaye katika siku za karibuni, amekuwa Palestina na Israel, kwa ajili ya kushiriki katika baadhi mambo muhimu ya Hija ya Papa Francisko katika Nchi Takatifu.
Ombi lake kwa Waarabu Wakristo wa Palestina, alilitoa Jumanne iliyopita, wakati wa Ibada ya Misa, katika Parokia Katoliki ya Mama yetu wa Fatima ya Beit Sahour , karibu na Bethlehem. "Kaeni katika nchi yenu , na kukabiliana na changamoto kwa pamoja," alisema Patriaki Rai na kuwataka kila mtu kukikataa kishawishi cha kutaka kuuza ardhi badala waihifadhi kwa ajili ya urithi huu wa thamani , hata kwa gharama ya sadaka ."

Siku ya Jumapili Patriarki Rai alikutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas , ambako Patriarki alipewa kuwa tuzo ya "Nyota ya Yerusalemu" ambayo ni ishara ya heshima ya juu inayotolewa na Mamlaka ya Palestina, kwa mtu aliyefanya zaidi kulisadia taifa la Palestina. Patriarki Rai, ametunukiwa heshima hiyo kwa ajili ya ujasiri wake katika kutetea eneo la Nchi Takatifu , kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyotolewa na uwakilishi wa Palestina nchini Lebanon. “Ni nani hataki amani katika Palestina, " alihoji Patriaki Rai, wakati akikutana na Rais wa Palestina. NI nani hataki amani Mashariki ya Kati. "

Patriaki Rai ni kiongozi wa kwanza wa dini mahalia nchini Lebanon na eneo la Israel tangu mwaka 1948 , mwaka wa kuundwa kwa serikali ya Isralel ya Wayahudi. Lebanon iliionyesha upinzani wa uamuzi wa Patriki Rai, kuwa na mahusiano na nchi ambayo wao walikuwa hawajatia saini mkataba wa amani, baada ya migogoro ya miongo kadhaa iliyopita. Kadi. Rai alitetea sababu ya uchaguzi wake , akisema yeye alitaka kutembelea Nchi Takatifu kama Mkristo katika eneo hilo lenye kwa na mizizi ya Ukristo. Patriaki Rai aliyepokea idhini ya kusafiri toka Mamlaka ya Kiraia ya Lebanon, alitembelea Parokia ya Maronite ya Yopa, Nyumba ya watawa ya Latrun Yerusalemu ya Mashariki na mwisho wa wiki, ana mpango wa kukutana na jamii ya Lebanon wanaoishi eneo la Galilaya. Israel inakadiriwa kuwa na Wakristu 11,000 Maronite . 

No comments:

Post a Comment