Tunu
msingi za maisha ya ndoa na familia ni kiini cha tafakari kama sehemu
ya maandalizi ya Siku kuu ya Mtakatifu Anna, Mama yake Bikira Maria,
ambayo kwa mwaka huu inaadhimishwa kwa namna ya pekee kabisa, wakati
huu Mama Kanisa anapoendelea kujiandaa kwa ajili ya maadhimisho ya
Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya Familia, yatakayofanyika mjini
Vatican kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 19 Oktoba 2014.
Katika Parokia ya Mtakatifu Anna iliyoko mjini Vatican, waamini wameanza Sala kwa ajili ya maandalizi ya Siku kuu ya Mtakatifu Anna, kwa kusali na kuwaombea watoto, wanawake na wazee. Padre Bruno Silvestrini, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Anna mjini Vatican anasema kwamba, kipindi hiki cha siku tatu hadi kilele cha maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Anna, waamini Parokiani hapo wanasali na kutafakari kuhusu tunu msingi za maisha ya ndoa na familia. Ni kipindi cha kushuhudia Injili ya Familia, ili kurithisha tunu hizi kwa vijana wa kizazi kipya.
Anasema, wanawake wajawazito wanaendelea kusali kwa ajili ya kumwomba Mtakatifu Anna ili awasaidie kupata utulivu katika shida na mahangaiko yao ya ndani, ili hatimaye waweze kujifungua salama kadiri ya mapenzi ya Mungu na kuwalea watoto wao katika misingi ya Kikristo na utu wema.
Kilele cha maadhimisho haya ni hapo tarehe 26 Julai 2014 kwa Sala na Ibada ya Misa takatifu itakayoongozwa na Kardinali Angelo Comastri, Makamu Askofu, Mji wa Vatican. Ibada hii itafanyika wakati wa mchana. Jioni majira ya saa 12:00, Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Parokia ya Mtakatifu Anna, ili kwa maombezi ya Mtakatifu Anna, wanawake wajawazito waweze kujifungua salama na asaidie pia kulinda familia ambazo kwa nyakati hizi zinakabiliwa na misuko suko ya maisha.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment