Wednesday, August 20, 2014

Msalaba wa Kristo ni kiungo pekee katika kushinda fitina na kutengana.



Baba Mtakatifu Francisco , Jumatano hii akiwa Vatican , alitoa Katekesi kwa mhujaji na wageni katika ukumbi wa Paulo VI. Kwenye hotuba yake alirejea safari yake ya kitume, aliyoifanya Korea Kusini kwa muda wa siku tano ambayo alikamilisha Jumatatu ya wiki hii. Aliitumia nafasi hii kurudia kutoa shukurani zake kwa Bwana akisema”Ninamshukuru Bwana kwa ajili ya zawadi hii kubwa”, ambamo nimeweza kutembelea kanisa pevu na lenye nguvu, lililosimikwa katika ushuhudi wa mashahidi wafia dini na lililohamasishwa na roho ya kimisionari, katika nchi ambamo walikutana na utamaduni za kale wa Asia na kupandikiza mbengu ya kudumu ya Injili.

Na pia aliitumia nafasi hii ya katekesi kurudia kutoa shukrani zake kwa wapendwa Maaskofu wa Korea, na Rais wa Jamhuri ya Korea Kusini , na Mamlaka nyingine za Kitawala na kwa wale wote ambao walio fanikisha kazi na huduma kwa ajili ya ziara yake. Papa alitaja umuhimu wa safari hii ya kitume, akibainisha kwamba, ilikuwa na maneno makuu matatu, kumbukumbu, matumaini, ushuhuda.

Na aliigusia historia ya Jamhuri ya Korea kwamba, ni nchi ambayo imekuwa na maendeleo ya kiuchumi ya kasi sana na watu wake ni wafanyakazi hodari na wenye nidhamu katika lengo la kudumisha nguvu na urithi kutoka kwa mababu zao

Kwa azima hiyo, Kanisa limekuwa ni mlezi wa kumbukumbu na matumaini, ni familia ya kiroho ambayo kwayo , watu wazima, hurithisha kizazi kipya, vijana, mwanga wa imani waliopokea kutoka kwa wahenga wao, na katika kutunza kumbukumbu ya mashahidi wa zamani wa imani ,na kuwa ushuhuda mpya, kwa sasa na kwa matumaini ya baadaye. Kwa mtazamo huu, Papa ametaja safari yake imekuwa na matukio kuu mawili : Ibada ya kuwataja kuwa wenye Heri Mashahidi wa Dini wa Korea 124, licha ya wale 30 waliokwisha tajwa kuwa Watakatifu miaka 30 iliyopita na Mtakatifu Yohana Paulo II; na pili ni mkutano na vijana,katika adhimisho la Sita la Siku ya Vijana barani Asia.
Papa alirejea tukio hilo akisema ,kijana daima hutaka kufahamu habari za mambo yanayomzunguka na ni mtu aliyejaa uzima tele na ushuhuda wa kweli wa majitolea ya thamani ya maisha, humwonyesha njia ya kweli katika maisha ya mtu. Papa alizungumzia Ukweli huu kwamba, ni Upendo, ni Mungu ambaye alichukua mwili katika Yesu, shahidi kwanza wa Mungu. Na amemshukluru Mungu kwamba, katika safari zake mbili kwa ajili ya vijana, Roho wa Bwana Mfufuka aliwajaza vijana furaha na matumaini, ambayo vijana wanaipeleka katika mataifa yao. Papa anatazamia vijana hao,watafanya mambo mengi nzuri!

Papa aliendelea na maelezo yake akisema, Kanisa la Korea, pia linatunza kumbukumbu ya jukumu msingi la walei, katika kuwa wapanzi wa imani mpya, kimaisha na kupitia kazi za uinjilishaji. Papa ameona ukweli kwamba, katika nchi hiyo, jumuiya ya kikristo hazikuanzishwa na wamisionari kutoka nje, lakini na kundi la vijana Wakorea katika nusu ya pili ya mwaka 1700, ambao walivutiwa na baadhi maandiko ya Kikristo, na waliyasoma vizuri na kuchagua kuwa mwongozo wa kutawala wa maisha yao . Papa alieleza jinsi mmoja wao alivyotumwa kwenda Beijing kupokea Ubatizo na baada ya kubatizwa alirudi na kuwabatiza wenzake. Kutoka katika kikundi hiki cha mwanzo , kulichipuka jumuia kubwa ambayo tangu mwanzo wa karne ya dhuluma na mateso na vurugu, Wakristo hao hawakupoteza imani na maelfu kuwa mashahidi wa dini. . Kwa hiyo, Kanisa katika rasi ya Korea, limejengwa juu ya imani, inayoonekana katika safari na ushuhuda wa waamini walei.

Baba Mtakatifu kwa kuiangalia historia ya imani Korea amesema, kuwa Mkristo hakumwondolei mtu utamaduni wake, wala kukandamiza haki za binadamu katika maisha ya kila siku, kama ilivyo kuwa karne na karne, lakini humwezesha kutembea kwa amani katika kuutafuta ukweli na kutenda kwa upendo wa Mungu kwa jirani. Na ndivyo, Kristo hamtelekezi mtu bali humkubatia kwa wema na kumwelekeza katika ukamilifu. Lakni hili linahitaji kufahamu kwamba ni kumweka mbele Kristo katika kupambana na kushinda mabaya, yenye kuleta ugomvi kati ya mtu na mtu, na kati ya taifa na taifa. Ni kukataa kutengwa na nguvu za ibada ya sanamu ya fedha, ambayo humwanga sumu kali hasa katika mioyo ya vijana.

Papa alisema, Kwa mtu kukataa hayo, hupata ushindi wa kusema ndiyo kwa Yesu Kristo, aliyeyashinda maovu kwa sadaka yake ya upendo. Na hivyo, hata sisi ni lazima kuwa imara , na kubaki katika Yeye, katika upendo wake, wenye kutuwezesha kuwa mashahidi, tukiishi kwa kushuhudia ushindi wake. Na imani hii, tunaiomba daima, na sasa tunaoiomba kwa ajili ya vijana wote wa dunia na Korea, ambao wanakabiliwa na madhara ya vita na mgawanyiko, ili waweze kutembea pamoja kaika safari ya udugu na maridhiano.

Baba Mtakatifu alikamilisha maelezo yake kwa kusema, safari yake yake nchini Korea, ilimulikiwa na mwanga wa Sikukuu ya Maria Kupalizwa Mbinguni. Mama bikira Maria, tokea juu alikoketi karibu na Kristo Mfalme, Mama wa Kanisa anaambatana na safari ya watu wa Mungu, yaani Kanisa, akiwadumisha katika hatua zote za kucosha na ngumu , akiwafariji katiak majaribu na kufungua upeo macho ya matumaini. Kwa maombezi yake. Mzazi wa Bwana, siku zote amewabariki watu wa Korea, zawadi ya amani na ustawi; na kubariki Kanisa katika nchi hii, kwa sababu daima limekuwa thabiti na limejaa furaha ya Injili.
Katika siku ya mwisho ya ziara yake ya Korea, Papa Francisco, aliongoza Ibada ya Misa, kwa nia ya kuomba amani na maridhiano katika Rasi ya Korea. Papa aliomba neema ya uponyaji na umoja ishinde moyo unaoigawa Rasi ya Korea. Katika mwanzo wa Misa hiyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Seoul, Myeong –dong- mapema siku ya Jumatatu, Papa pia, aliomba msaada kwa ajili ya kundi la wazee wanawake 'faraja wanawake' walio tekwa wakati wa vita kuu dunia na kuingizwa ktika utumwa wa kingono , kwa ajili ya kuwafurahisha wanajeshi wa Kijapani.

Katika hotuba yake Papa Francis alikumbuka mgawanyiko na migogoro ambayo umedumu kwa zaidi ya miaka sitini, kati ya Korea Kusini na Korea ya Kaskazini, vya tangu miaka ya 1950 kwa kuwataka wafuasi wote wa Kristo katika Korea kutafakari juu ya mchango wao wenyewe kwa ujenzi wa ukweli tu na jamii yenye ubinadamu.
Papa alisema ahadi ya Mungu kwa watu wake, inatoa changamoto kwetu kama waamini kujichunguza wenyewe uwajibikaji wetu , kwa wale wasiobahatika kufanikiwa kama sisi wenyewe. Na pi ani changamoto kwa Wakristo wa Korea , kuwa imara katika kukataa mawazo yote yenye kuwa na umbile la kujenga fitina, mashaka, tuhuma, ushindani na mapambano, badala yake, wajenge utamaduni kwa mujibu wa mafundisho ya Injili na uadilifu bora wa jadi ya nchi yao. Na kuzjingatia kwamba Ni msalaba pekee wa Kirsto wenye kuwa na uwezo wte , na ndilo daraja katika kila mgawanyiko na uponyaji wa majeraha.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment