Friday, October 3, 2014

Mkutano wa Mabalozi kutoka nchi za Mashariki ya Kati na Wakuu wa Curia ya Roma


Mabalozi toka nchi za Mashariki ya Kati katika Jimbo Takatifu, watakuwa na Mkutano utakaoanza Alhamis 2-4Oktoba. Na washiriki wa mkutano huo ni Balozi kutoka Misiri, Yerusalem, Palestina, Jordan, Iraq , Iran , Libano, Siria , Uturuki, pia wawakilishi wa kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, na Gineva kwa upande wa Ulaya.
Na Vatican watakaohudhuria kikao hicho ni Makatibu wa idara za Curia ya Roma, Katibu Mkuu wa Vatikan , Katibu msaidizi wa mahusiano ya nchi a nje , vilevile Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, ambaye alitumwa na Baba Mtakatifu hivi karibuni kutembelea maeneo yaliyo na vurugu na ghasia za kivita Mashariki ya Kati, pia wahusika wakuu katika Baraza la Kipapa hasa Usharika wa Makanisa ya Mashariki ya kati, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini, na Baraza la kipapa la haki na amani.
Baba Mtakatifu Fransisco atasalimia wajumbe wa mkutano huu, Alhamisi 2 Octoba wakati wa kufungua mkutano wao utakaomalizika Jumamosi 4Octoba asubuhi.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment