Wafiadini
Wakatoliki
Kati yao wanajulikana na kuheshimiwa
duniani kote kwa namna ya pekee Wakatoliki 22 waliokuwa wahudumu wa ikulu
ya kabaka wa Buganda Mwanga II
(1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885
na tarehe 27 Januari 1887
kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya
kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika
walioandaliwa na kardinali Charles
Lavigerie.
Ndio wafiadini wa kwanza wa kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu. Majina yao ni haya:
- Yosefu Mukasa Balikuddembe († Nakivubo, 15 Novemba 1885), wa ukoo Kayozi, wa kwanza kuuawa akiwa na miaka 25.
- Andrea Kaggwa († Munyonyo, 26 Mei 1886), wa kabila la Banyoro, ndugu wa mfalme.
- Ponsyano Ngondwe († Ttakajjunge, 26 Mei 1886), wa ukoo Nnyonyi Nnyange.
- Dionisi Ssebuggwawo († Munyonyo, 26 Mei 1886), wa ukoo Musu.
- Atanasi Bazzekuketta († Nakivubo, 27 Mei 1886), wa ukoo Nkima.
- Gonzaga Gonza († Lubowa, 27 Mei 1886), wa ukoo Mpologoma, kabila la Basoga.
- Matias Mulumba Kalemba († Kampala, 27 Mei 1886), wa kabila la Banyoro, ukoo Lugave.
- Noe Mawaggali († Mityana, 31 Mei 1886), wa ukoo Ngabi.
- Karolo Lwanga († Namugongo, 3 Juni 1886), wa ukoo Ngabi. Pamoja naye waliuawa hawa wafuatao:
- Luka Banabakintu (miaka 35), wa ukoo Mmamba;
- Yakobo Buzabaliawo (miaka 25), wa ukoo Ngeye;
- Gyavira Musoke (miaka 17), wa ukoo Mmamba;
- Ambrosi Kibuka (miaka 18), wa ukoo Lugave;
- Anatoli Kiriggwajjo (miaka 20), wa kabila la Banyoro;
- Mukasa Kiriwawanvu (miaka 20), wa ukoo Ndiga;
- Achile Kiwanuka (miaka 17), wa ukoo Lugave;
- Kizito, kijana kuliko wote, kwa kuwa alizaliwa mwaka 1872, wa ukoo Mmamba;
- Adolfo Mukasa Ludigo (miaka 24), wa kabila la Banyoro;
- Mugagga Lubowa (miaka 16), wa ukoo Ngo;
- Bruno Sserunkuma (miaka 30), wa ukoo Ndiga;
- Mbaga Tuzinde (miaka 17), wa ukoo Mmamba.
- Yohane Maria Muzei, mzaliwa wa eneo la Kagera (Tanzania ya leo), wa mwisho kuuawa († Mengo, 27 Januari 1887) akiwa na umri wa 30.
Habari kwa hisani ya wikipedia
No comments:
Post a Comment