Wednesday, December 2, 2015

Onesheni utashi wa kutaka kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani!




Askofu mkuu Dieudonnè Nzapalainga wa Jimbo kuu la Bangui baada ya kuzindua maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu, Jumapili ya kwanza ya kipindi cha Majilio, hapo tarehe 29 Novemba 2015, tukio la kihistoria lililofanywa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake ya kitume Barani Afrika alikaza kusema chuki, vita na uhasama ni mambo yanayokinzana na Injili ya uhai! Haya ni majanga makuu yanayomwandama mwanadamu katika hija ya maisha yake hapa duniani.
Askofu mkuu Nzapalainga anawahamasisha waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuwa mashuhuda wa imani inayomwilishwa kwatika matendo hasa wakati huu wanapokabiliwa na vita, kinzani na mipasuko ya kidini na kisiasa; waamini wanapaswa kusimama kidete kushuhudia imani ya kwa Kristo na Kanisa lake pamoja na kukataa kishawishi cha kutumbikia katika hali ya kutaka kulipiza kisasi kama njia ya kujipatia haki binafsi.
Licha ya shida na magumu mbali mbali yanayoendelea kuliandama Kanisa katika maisha na utume wake, lakini bado kuna Wasamaria wema wanao lisaidia Kanisa kutekeleza dhamana na utume wake miongoni mwa maskini, ili kuwatangazia watu Injili ya upendo inayojikita katika matendo ya huruma kimwili, mambo msingi katika maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu.
Bado kuna mambo mengi ya kutekeleza, huu ni wajibu endelevu wa waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, wanaliwezesha Kanisa kwa hali na mali ili liweze kuendelea kuwa kati ya watu kwa ajili ya watu kwa njia ya huduma makini. Kanisa Katoliki Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati linajielekeza zaidi katika utume kwa vijana na familia kwani wao ndio waathirika wakubwa wa vita na mipasuko ya kijamii.
Baba Mtakatifu Francisko kwa kufungua lango la maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu Jimboni Bangui, ameonesha ujasiri mkubwa wa imani na kwamba, hii ni zawadi kubwa kwa Familia ya Mungu Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati kuhakikisha kwamba, wanaambata fadhila ya imani, matumaini na mapendo; tayari kuendeleza mchakato wa haki, amani na upatanisho, changamoto kubwa kwa nyakati hizi. Lango la Jubilei ya huruma ya Mungu ni lango la: matumaini, msamaha, upatanisho na maisha mapya.
Hii ni changamoto kwa waamini kutambua udhaifu wao, tayari kukimbilia huruma na upendo wa Mungu kwa njia ya toba na wongofu wa ndani. Kwa kufanya hivi katika hali ya unyenyekevu wataweza kuwa na ujasiri wa kumwendea Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo anakaza kusema Askofu mkuu Nzapalainga ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kukoleza mchakato wa haki, amani, msamaha na upatanisho nchini humo. Amekazia kwa namna ya pekee umuhimu wa sakramenti ya Upatanisho kama chemchemi ya upatanisho kati yao na Mwenyezi Mungu. Kwa njia hii waamini wataweza kuwa kweli wamefahamu maana na umuhimu wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu katika maisha yao!

Habari kwa idhini ya Radio Vatican.

1 comment:

  1. As claimed by Stanford Medical, It's really the SINGLE reason women in this country live 10 years longer and weigh 42 lbs lighter than us.

    (Just so you know, it is not related to genetics or some secret exercise and really, EVERYTHING about "how" they are eating.)

    BTW, What I said is "HOW", not "what"...

    Tap on this link to find out if this brief quiz can help you find out your real weight loss possibility

    ReplyDelete