Thursday, April 17, 2014

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bassangoa ameachiliwa huru!



Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yenye makao yake makuu mjini Roma ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikijikita katika mchakato wa haki, amani na upatanisho nchini Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Alhamisi, tarehe 17 Aprili 2014 imetangaza kwamba, Askofu Dèsire Nongo Aziagbia wa Jimbo Katoliki Bossangoa, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati aliyekuwa ametekwa nyara na watuwasiojulikana siku ya Jumatano, ameachiwa huru.

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya kati limekuwa mstari wa mbele katika mchakato wa upatanisho wa kitaifa nchini humo pamoja na kuendelea kuwasaidia wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi ambao idadi yao inaendelea kuongezeka siku hadi siku.

Askofu mkuu Dieudonnè Nzapalainga wa Jimbo kuu la Bangui amemshukuru Mungu kwa hatua hii iliyofikiwa na kwamba, Kanisa lina matumaini kuwa mchakato wa haki, amani na upatanisho wa kitaifa utaendelea ili kujenga na kudumisha misingi ya amani na utulivu. 

habari kutoka radio vatican

No comments:

Post a Comment