Thursday, April 17, 2014

Upadre ni zawadi isiyopokonywa,na hudumu milele- Papa.



Alhamisi Kuu, Makanisa Katoliki Duniani Kote, yameadhimisha Ibada za Misa ya Krisma na Karamu ya mwisho ya Bwana. Mapema Alhamisi , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, Baba Mtakatifu Francisko, aliongoza Ibada ya Misa ya kubariki mafuta ya upako Mtakatifu “ Krisma” , akisaidiana na Makardinali , Maaskofu na Mapadre wa Jimbo la Roma.
Katika homilia yake , alikumbusha umuhimu wa adhimisho la Alhamisi Kuu, kwamba ni siku inayoonyesha jinsi Kristo, alivyoupenda Ulimwengu bila kipimo (taz. Yn 13:01 ). Na ni siku ya furaha kwa decania ya Mapadre , kukumbuka ahadi yao katika utumishi wa kikuhani katika shamba la Bwana. Bwana amewapaka mafuta, mafuta ya furaha katika Kristo, upako unao waalika kupokea na kuchukua, malipo ya zawadi kubwa ya furaha , furaha ya kuwa Padre. Furaha hii ya ukuhani ina thamani sana , si tu kwa ajili yao mapadre lakini pia kwa watu wote waaminifu wa Mungu , waaminifu wanao mzunguka Padre aliye katikati yao , aliyeitwa na kupakwa mafuta na Bwana na kutumwa kwao.
Papa aliendelea kueleza juu ya Mafuta ya furaha kwamba ni Furaha ya ukuhani ambamo mna chanzo cha upendo wa Baba , na Bwana anatamani kuona kwamba furaha ya Upendo huu ipo ndani mwa Mapadre katika ukamilifu kamili (Yn 15:11). Papa alieleza na kuendelea kuitafakari furaha hii akielekeza fikira pia kwa Bikira Maria , Mama wa Injili hai, chanzo cha furaha kwa watoto wadogo kama ilivyolezwa katika waraka wa Kichungaji wa( “ Evangelii gaudium “, 288 ). Papa anaona si kutia chumvi, kusema Padre ni mtu ndogo sana , ikilinganisha na kipimo cha ukuu wa zawadi aliyopewa ya kuhudumu kati ya watu maskini. Padre ni maskini zaidi katika watu wote maskini, kama hakutajirishwa na Yesu katika umaskini wake. Ni mtumishi asiyekuwa na maana kati ya watumishi, iwapo hana wito kwa Yesu , na ni mjinga kati ya wajinga wengi, iwapo Yesu si mshauri wake , na kiwapo hana uvumilivu kama Petro alivyokubali taratibu kufundishwa na Yesu.
Papa aliendelea kuelekeza, “Mapadre ni wanyonge zaidi ya Wakristo kama hawakubali kuimarishwa na Kristo Mchungaji Mwema. Hakuna aliye ndogo kuliko Padre aliyeaguka katika mambo yake mwenyewe. Kwa hiyo, sala ya ulinzi dhidi ya mashambulizi yote ya Shetani, ni sala kwa Mama Bikira Maria: inayosema, Mimi ni Padre kwa sababu Yeye kwa wema wake ameuona unyonge wangu. (cf. Lk 1:48 ). Na katika unyonge huu mnapatakana furaha ya Upadre”.

Papa amesema, kwake yeye kuna mambo muhimu matatu katika furaha yao ya kikuhani , Ni furaha ya kuwa mmoja wa waliopakwa mafuta , si mpako wenye kusiriba kiburi , hasira na chuki ),lakini ni furaha isiyoharibika, ni furaha ya kimisionari yenye kusambaa kwa wote na kuwavutia wote, ikianzia na walio mbali sana hadi kwa walio karibu zaidi. Kwa hiyo ni furaha ya upako, furaha isiyoharibika na furaha ya kimisionari.

Na kwamba ni furaha ya Upadre isiyokuwa na mwisho. Ni zawadi ya Uadilifu ambayo hakuna mtu anaweza kuichukua mbali au kuongeza kitu chochote, kwa kuwa ni chanzo cha furaha usio na mwisho : furaha isiyoharibika , ambayo Bwana ameahidi kwamba hakuna mtu anayeweza kuchukua (taz. Yn 16:22). Inaweza kulala au kufifishwa na dhambi au na wasiwasi wa maisha, lakini bado haiwezi kutoweka, itaendelea kuwepo katika kina cha chini kama makaa ya moto uliofunikwa chini ya majivu, na bado unaweza kuwaka upya.( 2 Tim 1:06 ). Furaha ya ukuhani, huandamana daima na uaminifu na utii.
Baba Mtakatifu Francisko katika homilia yake , amemwomba Bwana, kuwawezesha vijana wengi , kuigundua hamu kubwa iliyomo ndani ya mioyo yao , inayowaita kwa nguvu kutoa jibu la ndiyo katika kumtumikia Bwana kwa maamuzi thabiti. Pia Papa, ametolea sala kwa ajili ya Mapadre wapya , ili waweze kusonga mbele na ukuhani wao katika dunia ya leo , kujitola kikamilifu kati ya watu wa Mungu , wakati wanapo furahia kuadhimisha kwa mara ya kwanza Ibada ya MIsa , homilia ya kwanza, ubatizo kwa mara ya kwanza na kuungamisha kwa mara ya kwanza.
Na kwamba Alhamisi Kuu, ni Siku ya kumwomba Bwana Yesu, aendelee kuimarisha furaha ya kikuhani kwa wale ambao wana miaka mingi katika utumishi huu. Ili Furaha hiyo isitengamana katika upeo wao wa macho , iwe ni furaha tupu kubeba mzigo wa wale wanao lemewa na huduma, na kwa makuhani wale ambao tayari wana uzoefu wa kazi za kichungaji , wapate kuimarika na kukusanya nguvu upya katika kupambana na mabadiliko ya nyakati . Bwana na adumishe kwa kina hekima na ukomavu wa furaha waliyo nayo Mapadre wazee kama Nehemia alivyosali “furaha ya Bwana ni nguvu zangu “(cf. Neh 8:10) .

Mwisho wa homilia yake Papa , kwa namna ya pekee akisema, katika Siku Kuu hii ya Makuhani, alimuomba Bwana Yesu, awaangazie vyema katika kuiona furaha ya Mapadre wazee , iwe kwa wale wenye afya njema au wagonjwa. Ni furaha ya Msalaba , inayo chipuka kutoka katika ufahamu kwamba, wana hazina isiyoharibika katika vyungu vya udongo. Papa amewatakia mapadre wote wazee mahali popote walipo kuwa na furaha na uzoefu wao katika njia hii kwa miaka mingi , iwe ni onjo la milele.. Na wajisikie kuwa na furaha ya kuwa na mwanga wa kuwamulikia watoto wao wa kiroho, kufurahia ahadi za kutoka mbali kwa tabasamu na upole, ahadi, kwa tumaini lisilo tahayarisha. Baba Mtakatifu Francisko , majira ya jioni anaongoza Ibada ya Karamu ya mwisho wa Bwana amb amo pia ataonyesha kama ishara ya huruma na unyenyekevu kwa kuwaosha miguu watu kadhaa. Ibada hii inafanyika katika Kituo cha kuhudumia watu walemavu , wagonjwa na wahitaji cha Shirika la Don Gnocci , cha hapa Roma.


habari kwa hisani ya vatican radio


No comments:

Post a Comment