MT.MAKSIMILIANO KOLBE UTUOMBEE ! |
Majitoleo kwa Imakulata aliyofundisha Mt.
Maksimiliano Kolbe kwa maneno na mfano wa maisha yake, ni aina ya ibada
bora kwa Mama wa Mungu.
Kujitolea kwa Imakulata ni kumtolea zawadi ya nafsi binafsi, ni kumtolea mawazo, maneno na matendo yote, ni kujitahidi kuishi jinsi Imakulata angeishi akiwa kwenye nafasi yangu, yaani ni kutimiza kwa uaminifu Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu wa hali ya kila mmoja.
Kwa tendo la kujitolea tunakuwa mali ya Maria Imakulata. Yeye anasafisha mawazo, maneno na matendo yetu na kuyatolea kwa Yesu: “Hivyo yatakuwa bila kasoro, safi. Na yakipata thamani kubwa kwa njia ya Umungu wa Yesu, yatamtukuza Mungu Baba kwa heshima” (Mt. Maksimiliano).
Ibada ya kujitolea kwa Bikira Maria Imakulata inaweza kuwa ya binafsi au ya hadharani.
Ibada ya binafsi ya kujitolea kwa Imakulata
Anayetaka kujiotolea kwa Bikira Maria Imakulata kabisa ndani ya chama cha “Ushujaa wa Imakulata”, ajichagulie mwenyewe siku, mahali na utaratibu wa kuonyesha uamuzi wake. Ni vizuri ibada hii ifanyike katika mojawapo ya sikukuu za Bikira Maria, baada ya kujiandaa kwa mfano kwa siku ya sala na kusoma juu ya Imakulata na utaratibu wa chama cha “Ushujaa wa Imakulata”, halafu kuungama na kushiriki katika Ekaristi Takatifu, akiwa katika hali ya neema. Baada ya hayo au kanisani au nyumbani asali sala ya kujitolea kwa Imakulata iliyoandaliwa na Mt. Maksimiliano: “Ee Imakulataa, Malkia mbingu na dunia...”.
Ishara ya nje ya kujitolea kwa Imakulata ni kuvaa Medali ya Muujiza, ambayo ilipendezwa na Imakulata mwenyewe wakati alipomtokea Mt. Katherina Laboure mwaka 1830: “Atakayeivaa atapata neema nyingi”. Kwa hiyo pia Mt. Maksimiliano aliichagua iwe ishara ya kujitolea kwa Bikira Maria ya wanachama wa “Ushujaa wa Imakulata”.
Kujitolea kabisa na kwa hiari kwa Imakulata ni sharti muhimu sana la kujiunga na “Ushujaa wa Imakulata”. Lakini ili kujiunga na chama hiki kikamilifu, kila mmoja anapaswa kutuma ombi la kuandikishwa kwenye kitabu cha wanachama. Ombi hili liwe na jina kamili, parokia, anwani (kwa ajili ya mawasiliano) na tarehe ya kujitolea.
Vivyo hivyo familia nzima inaweza kujitolea kwa Imakulata kwa pamoja na kujiunga na chama cha “Ushujaa wa Imakulata”, lakini wakati tu ambapo kila mwanafamilia atajitolea kwa hiari bila kulazimishwa hata kidogo.
Watoto wanapaswa kwanza kuandaliwa kiroho na wazazi. Halafi siku ya sikukuu ya Bikira Maria wote waungame na kushiriki katika Ekaristi Takatifu na kupokea Komunyo Takatifu wakiwa kwenye hali ya neema ya Mungu. Halafu wasali kwa pamoja au kanisani au nyumbani mbele ya picha au sanamu ya Bikira Maria, sala ya kujitolea kwa Imakulata, na baada ya hayo wavalishane Medali za Muujiza, ambazo tangu wakati huo zitakuwa ishara ya kuwa mali ya Maria Imakulata. Kisha wasali kwa pamoja au rozari au Litania ya Bikira Maria au sala nyingine. Sala hizo zote ziendane na uamuzi kwamba watajitahidi kuendelea kutimiza mpango wa “Ushujaa wa Imakulata” yaani “kufanya kazi kwa ajili ya uongofu wa watu wote kwa Mungu..., ili wote wawe watakatifu, chini ya ulinzi na kupitia kwa usuluhishi wa Bikira Maria Imakulata”, wakitumia njia za kitume: “Kusali, kufanya toba, kumtolea Mungu kazi za kila siku na mateso ya maisha; kumwomba Bikira Maria Imakulata kila siku kwa sala hii: “Ee Bikira Maria uliyekingiwa dhambi ya asili, utuombee sisi tunaoukimbilia ulinzi wako, na wale wote ambao hawaukimbilii ulinzi wako, hasa maadui wa Kanisa Takatifu na waliokabidhiwa kwako.”; kutumia njia zote halali kwa ajili ya kuwaongoza na kuwatakatifuza watu, kufuatana na uwezo binafsi katika hali mbalimbali ya kila mmoja na mazingira ya maisha yake, kwa kadiri zinavyojitokeza katika nafasi mbalimbali. Hizo zinaaminishwa kwa shauku na busara za kila mmoja. Njia zinazopendekezwa hasa ni: kueneza Medali ya Muujiza na utume unaoonyeshwa kwa mfano, neno na vyombo vya habari vya chama cha MI (k.f. Gazeti la ‘Shujaa wa Imakulata’)”.
Kisha majina yote yatumwe kwa ajili ya kuandikishwa kwenye kitabu cha wanachama cha “Ushujaa wa Imakulata”.
Familia ambayo inajitolea kabisa kwa Maria Imakulata, inapaswa kujenga Kanisa ya kifamilia linaloongozwa na upendo na mafundisho ya Yesu. Wanafamilia watajitahidi kutunza kati yao mazoezi ya kiroho na ibada kwa Bikira Maria, hasa zinazopendekezwa na Kanisa: sala ya rozari, sala ya Malaika wa Bwana..., Novena mbalimbali hasa kabla ya Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili (8 Desemba), kusoma Biblia na vitabu mbalimbali vya kikatoliki. Uwezo wa Maria wa kuitakatifuza familia utakuwa mkubwa zaidi kama kila mwanafamilia atajitahidi kuwa na uhusiano hai na Mwanae Yesu Kristo.

Habari kwa hisani ya shujaa imakulata
No comments:
Post a Comment