Baba
Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, mara baada ya maadhimisho ya Ibada
ya Misa Takatifu kwa ajili ya Siku kuu ya Bikira Maria Kupalizwa
mbinguni mwili na roho, hapo Jumatano, tarehe 15 Agosti, 2012, kwenye
Parokia ya Castel Gandolfo, alirejea tena wakati wa mchana, Ikulu ndogo
ya Castel Gandolfo, ili kusali sala ya Malaika wa Bwana.
Baba Mtakatifu alifanya rejea kwa Mapokeo ya tangu mwanzoni mwa Karne ya tano yanayoonesha Ibada kwa Bikira Maria aliyeonekana katika utukufu kwa kupalizwa mbinguni, lakini zaidi ile Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, iliyojidhihirisha kwa namna ya pekee wakati wa maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Efeso, kunako mwaka 431, ulipotamka kwamba, Bikira Maria ni Mama wa Mungu, kuwa ni sehemu ya Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Waamini wa Kanisa la Mashariki kwa miaka mingi walikuwa wanaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni kwa kielelezo cha kulala usingizi "Dormitio".
Fumbo la Bikira Maria kupalizwa mbinguni linakwenda sanjari na Fumbo la Pasaka, kiini cha ukombozi wa mwanadamu uliopatikana kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wa Kristo. Bikira Maria ni Tabernakulo ya kwanza ya Neno wa Mungu aliyefanyika mwili, hivyo anashirikishwa kwa namna ya pekee katika Fumbo la Pasaka na utukufu wa Kristo. Ni fumbo linaloonesha historia ya ubinadamu na matumaini ya waamini na Kanisa zima.
Bikira Maria aliyepalizwa mbinguni mwili na roho anaendelea kuliombea Kanisa ambalo bado liko safarini, ili liweze kupata neema ya uzima wa milele, anawalinda Watoto wa Kanisa ambao bado wako safarini bondeni huku kwenye machozi, ili waweze kufika salama mbinguni.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment