Monday, September 29, 2014

Hapana kubwa kutumia jina la dini kufanya ghasia na dhuluma.


Vatican Radio) Papa Francisko Jumapili alisema, hakuna mtu anayeweza kusema ana haki ya kumtumia Mungu kama silaha katika mipango ya utendaji wa dhuluma, vurugu na uonevu. Na pia asiwepo mtu wa kutumia kisingizio cha dini au jina la Mungu katika utendaji wowote dhidi ya heshima ya binadamu na dhidi ya haki za msingi za kila mwanamume na mwanamke, juu ya yote, haki ya kuishi na haki ya kila mtu ya uhuru wa dini!

Papa alieleza katika hotuba yake aliyoitoa wakati akikutana viongozi nchini Albania( Rais, Serikali, Mamlaka za Kiraia na Mabalozi na wanadiplomasia), Jumapili mara tu baada ya kuwasilia Albania, katika ziara yake ya Kitume ya siku moja. Hotuba aliyoitoa katika Jengo la Rais la Tirana, mkutano uliofanyika katika mazingira ya kufurahiana,kuthaminiana, hewa ya heshima na kuaminiana, katika mchanganyiko wa kitaifa wa Wakatoliki, Waotodosi na Waislamu. Ilikuwa ni wasaa uliotawaliwa na amani, mshikamano na ushirikiano kati ya wafuasi wa dini mbalimbali, kama zawadi ya thamani sana kwa nchi ya Albania.

Papa alizungumzia heshima kwa haki za binadamu, uhuru wa dini na uhuru wa kujieleza kwamba, ni kwa ajili ya kuruhusu ubunifu na shauku katika uwezo wa binadamu lakini wenye kuzingatia utu, ili kwamba iwe ni kwa ajili ya manufaa ya wote - Papa alieleza na kusifu uzoefu wa maisha machanganyiko ya Albania akisema inaonyesha kwamba, amani na matunda mshikamano kati ya watu na jamii ya waumini wa dini mbalimbali si tu kuhitajika, lakini inawezekana na ni ukweli".

Papa Francisko pia aligusia changamoto mpya ambazo lazima kukabiliana nazo wakati huu dunia ikiwa katika mwelekeo wa utandawazi wa uchumi na utamaduni. Alitahadharisha, kila juhudi lazima zifanyike kuhakikisha kwamba, ukuaji wa uchumi na maendeleo, inakuwa ni kwa ajili ya kuhudumia wote na si tu kwa ajili ya manufaa ya kundi dogo la watu.

Maendeleo alisema, yatakuwa tu halisi na endelevu iwapo yanazingatia haki msingi kwa watu wote wakiwemo maskini na heshima kwa mazingira kama kiini cha moyo wa maendeleo yote. Pamoja na utandawazi wa masoko ni lazima utandawazi huo uende sambamba na mshikamano; na ukuaji wa uchumi ni lazima uwe na heshimu kubwa kwa viumbe; pamoja na haki za watu binafsi, lazima kuwe na haki za uhakika za kulinda wote wenye kuwa madaraja kati ya mtu binafsi na serikali na familia, Papa alisisitiza.

Na wakati Papa akiwa ndani ya ndege, safari kutoka Albaniahadi Roma, ambayo ilichukua muda wa dakika 90 tu, pia aliwapa wasaa wa kubarizi na kuhojiwa na waandishi wa habari.

Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari, Papa Francisko alisisitiza ukweli juu ya Albania, kwamba ni kati ya mataifa ya Ulaya yaliyo sahaulika pembezoni, na hivyo anatumaini ziara yake imeleta hisia hizo na hivyo taifa litaendelea kuinuliwa zaidi . Na kwamba, licha ya ukweli kwamba Albania ina idadi kubwa ya Waislam, lakini nchi hiyo haijiiti kuwa Nchi ya Kiislam, lakini ni nchi ya Ulaya, inayokuwa mfano mzuri unaoonyesha ushirikiano kati ya dini kuu tatu: Uislamu, Ukristo Orthodox, na Ukatoliki.

Papa alieleza umuhimu wa utamaduni wa kuishi pamoja, uvumilivu, na udugu katika nchi za Balkani. Na aliguswa zaidi na maelezo yao tangu mwanzo kwamba taifa dogo barani Ulaya ambalo bado changa, katika maana ya kuwa na utawala wa kidemokrasia, baada ya utawala wa kikatili wa kikomunisti na ukana Mungu. Kwa kipindi, Papa ilimlazimu kuisoma historia ya mateso ya watu katika taifa hilo, ya wakati wa zama za Kikomunisti, kujaribu kuelewa.Papa amekiri kuwa kulikuwa ni ni kipindi cha Ukatili wa kiwango cha juu cha kutisha,si tu Wakatoliki, lakini pia Orthodox na Waislamu ... hii ilitokea kwa sababu wao alisema wanaamini katika Mungu. Kila moja ya jumuiya tatu wamelieleza Mungu na sasa kuishuhudia udugu wao.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment