Monday, September 29, 2014

Papa ashukuru mapokezi mazuri ya Tirana Albania.


Katekesi ya Papa kwa mahujaji wageni kwa Jumatano hii mjini Vatican, imetafakari safari yake ya kitume katika Mji Mkuu wa Tirana Albania. Ziara ya siku moja lakini aliyoitaja kwamba, ilijaa utajiri mkubwa wa upendo na mshikamano kati ya Jimbo Takatifu na nchi ya Albania.

Katika Maelezo, Papa Francisco amesema, alikwenda Albania, kuonyesha mshikamano wake wa karibu na Kanisa zima na watu wa Albania, taifa ambalo kwa muda wa miaka mingi, liliteswa na kushamiri kwa ukana Mungu , na unyama wa serikali isiyojali uwepo wa Mungu. Baada ya kuangushwa kwa mamlaka hayo, sasa taifa linahitaji kupewa moyo, kwa ajili ya ufanikishaji wa kazi nyingi za kuijenga upya jamii, ili iwe ni jamii yenye kupenda amani na kuheshimiana na kushirikiana katika huduma, kwa ajili ya manufaa ya wote.

Papa ameonyesha kufurahi na kumshukuru Mungu, kwa uwepo wa roho ya mshikamano na mazungumzo kati ya jamii Albania licha ya tofauti za kidini na kitamaduni. Anamwoba Bwana, ili taifa hili lisonge mbela na roho huyo, na kamwe lisirudishwe nyuma katika mateso makali ya ukana Mungu. Papa alieleza kwa kuurejea Mkutano wake na viongozi wa dini mbalimbali, ambamo aliweza mwenyewe kuushuhudia moyo huo wa kuheshimiana na kushirikiana, uliojengwa juu ya utambulisho wa kila mmoja.

Papa Francisko, ameendelea kusema akiwa pamoja na ndugu zake katika Kristo wake kwa waume, waliweza kutoa heshima zao kwa ushuhuda wa kishujaa wa mashahidi wengi wa imani, ambao mateso yao sasa yanatoa matunda ya taifa kuzaliwa upya kiroho. Kwa ajili hiyo, Papa ametoa mwaliko kwa Wakristo wote, kuwa chachu ya wema, upendo na maridhiano katika jamii ya Albanian. Na ameomba msaada wa Mama Yetu wa Shauri Jema, Mungu aridhie kuendelea kuwasha mwamko na moto wa kujenga jamii ya haki, amani na Mshikamano, kwa Walbania wote..

Baba Mtakatifu francisko alikamilisha tafakari yake kwa kusalimia makundi mabalimbali ya mahujaji na wageni waliofika kumsikiliza wakiwemo wanafunzi wapya waliojiunga katika masono kwenye Taasisi ya Uingereza, kama wanafunzi wanao wania kuwa Mapadre. Papa aliwahakikishia wanafunzi hao kwamba, kiroho yu karibu nao,hasa wakati huu wanapoanza mwaka wa kwanza wa masomo kwa ajili ya Upadre. Pia alitaja makundi mengine yanayozungumza lugha ya Kiingereza wengi wakiwa kutoka Uingereza, Ireland, Scotland, Denmark, Norway, Uholanzi, India, China, Japan, Kenya, Australia, New Zealand, Canada na Marekani. Kwao wote aliwaombea furaha na amani ya Bwana Yesu. "Mungu awabariki"! 

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment