Monday, September 29, 2014

Uwepo wa Wakristo Nchi Takatifu, ni rasilimali watu


Patriaki Fouad Twal, Upatriaki wa Yerusalem ya Mashariki, amesema uwepo wa wahamiaji Wakristo katika Nchi Takatifu kwa sababu mbalimbali kama wafanyakazi na wafanya biashara na wachuuzi, ni sehemu ya utajiri wa kanisa na zawadi katika eneo hilo, kwa kuwa watu hao pia hushiriki ktika shughuli nyingine za kijamii zikiwezo za kisiasa. Patriaki wa Yerusalemu ya Mashariki Fouad Twal, ameonyesha kutambua mchango msingi wa jamii ya Wakristo wahamiaji ambao huendelea kuwakilisha kweli msingi na muhimu katika miji mingi ya Israel, kuanzia mjini wa Tel Aviv.

Patriaki Twal, alieleza haya mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifanya ziara ya kichungaji kwa Jamii ya Kikristo ya eneo la Jaffa , ambako alitaja uwepo wa Wakristo hao ni ishara muhimu ya heshima na shukrani kama ilivyoripotiwa na vyanzo rasmi ya Upatriaki. Patriaki Twal, akikutana na Wakristo wa eneo hilo, aliivutiwa na uvumilivu wa Wakristo jamii ya Hindi na Ufilipino, ambao ni jumuiya ya kikristo ya wahamiaji wanaoishi katika hofu ya kuwa kafara wa kufukuzwa katika maeneo waliyokimbilia na mahali wanapo ishi kwa pamoja. Akiwa katika eneo hilo la Jaffa, Patriaki aliwasisitiza umuhimu wa kujumuika pamoja ktiaka Ibada za Jumapili, kugundua manufaa ya ushirika miongoni mwa jamii mbalimbali kama chanzo cha utajiri wa kuheshimiana, na kutambua kwamba wao ni Kanisa moja, Kanisa la Mungu. 

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment