Wednesday, March 18, 2015

Zingatieni kanuni maadili


Rais, Jakaya Kikwete wa Tanzania amekemea vitendo vinavyotia aibu uteuzi wake, vya uevi kupindukia, madeni ya kupindukia na matumizi mabaya ya madaraka vinavyofanya na wakuu wa Wilaya nchini. Aidha, ni moja ya sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa baadhi ya wakuu wa wilaya aliokuwa amewateua. Kikwete alitoa, kauli hiyo, mjini hapa juzi wakati alipokuwa akifungua semina elekezi ya wakuu wa wilaya wapya 27, ya siku 4 inayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar, Dodoma.

Alisema, wakati mwingine anapopokea taarifa za mambo machafu yanayofanywa na wakuu wa wilaya katika maeneo yao amekuwa akitamani yasiwe ya kweli. Alisema, baada ya kuteuliwa wakuu hao wa wilaya wamekuwa wanatumia madaraka vibaya wakiwaonea wananchi ambapo mtu anapokosea kidogo tu anaamuru kuwaweka mahabusu. “Mkuu wa wilaya akiwa baa ndio mlevi kushinda watu wote, analewa mpaka anahitaji usaidizi wa kuinuliwa kwenye kiti, watu wanaamua kumuita mke wake nyumbani ajae kumbebe ni aibu sana,..

“Unakuta wana madeni kupindukia mitaani, wengine wakwapuaji tu mara amechonga laini hii mara hii, mkuu wa wilaya kama huyu ni vigumu sana kuendelea naye kwani anatuangusha,”alisema. Aliwataka, kutoka kufikika na kusikika kwa wanaachi na kuacha tabia ya kukaa maofisini wakizunguka kwenye vitu kwa madai kuwa nafasi zao ni muhimu sana.

“ Mmeteuliwa kuwatumikia wananchi na si vinginevyo, watu wanasumbuliwa sana, hivi vyombo vya serilikali vingine vinatesa sana kwa jina la vyombo hivyo ni lazima mkawasikiliza wananchi na kutatua kero zao,” alisema. Yeye kama rais ana mamlaka makubwa sana lakini hatumii madaraka yake vibaya iwaje wao wawe wanatoa amli za kuwaweka watu ndani bila sababu za msingi.

Rais, alisema, serikali ina majukumu matatu ambayo ni utawala, usalama na maendeleo amabyo huko wilayani yanasimamiwa na mkuu wa wilaya ambaye ndiye muwakilishi wa rais, anatakiwa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa sawa. Kuhusu utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio kipo madarakani, alisema si jambo la hiari wala muali kwa mkuu wa wilaya kutoa taarifa za utekelezaji kwa viongozi wa chama wanapozihitaji.

“Chama cha Mapinduzi ndiyo mtawala hivyo ni lazima ahoji nawe ni lazima utoe taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo kwenye vikao husika vya chama kila zinapohitajika,”alisema. Akizungumzia ujenzi wa maabara ambapo ameongeza muda mpaka Juni mwaka huu, aliwataka wakuu hao kutokuwa na kisingizio chochote kwamba ni wateuzi wapya bali wahakikisha muda unapofika maabara zimekamilika katika maeneo yao.

Dk. Kikwete, alisema si rahisi kumrudisha alietoka hivyo ni wajibu wao wapya kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya ujenzi wa maabara yalipofikia na kuweka msukumo wa kuhakikisha zinakamilika. Alisema, suala la ulinzi na usalama liko mikononi mwao, hivyo watumia kama mkono wao wa kuume kuhakikisha amani, utulivu, ulinzi na usalama katika maeneo yao unadumu. Kamati za ulinzi na usalama za wilaya ndio nguzo yao hivyo wakazitumie kwa utaratibu uliopo bila kuacha mana wasipokutana mara kwa mara kila mmoja ataendelea na mambo yake.

Wakati huo huo, Serikali ya Tanzania, imesema mwananchi ambaye atakuwa hajajiandikisha kwenye daftari wa kudumu la wapiga kura amepoteza fulsa kwani kitambulisho kinachotumika kwenye kura za maoni na uchaguzi mkuu ni kimoja. Kauli hiyo ilitolewa, mjini hapa jana na Rais Jakaya, Kikwete wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya semina elekezi kwa wakuu wa wilaya wapya 27.

Alisema, endapo mtu atagoma kuajiandikisha kwa maana amekatazwa na chama chake atakuwa amepoteza fulsa kwani hakuna fulsa nyingine tena. Aliwaagiza, wakuu hao kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuwaeleza umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lakini pia kujitokeza kwenye kura za maoni na kufanya maamuzi wanayoyataka.

Katika hilo aliwataka kutumia mamalaka yao ya ulinzi na usalama na kuhakikisha wananchi wanapata fulasa ya kuamua wanachoona kinafaa kwa uhuru.
“Naagiza chaguzi zote ikiwemo kampeni, zifanyika kwa amani na utulivu na hiyo ni kazi yenu, hakikisheni watu wenye nia mbaya wasipate mwanya wa kuharibu zoezi hilo na kugeuka kuwa fujo,” alisisitiza.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment