ROZARI
TAKATIFU YA MAMA BIKIRA MARIA
Anza
kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake
Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la
Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja
kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa
pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na
tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .
Baada
ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu)
fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo
ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
“Mungu Baba
utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu
Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria,
…..” Au;
“Utuongezee Imani ee
Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe
nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au;
“Salamu e
uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana,
Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Atukuzwe Baba, na
Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu,
utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni,
hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.
Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha
endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo
moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu
milele...” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni
mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya
Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi
linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA
ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu
na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli
anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie
unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu
anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya
jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa
Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa
hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu
hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne
na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka
jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la
dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa
kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za
uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa
miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua
Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa
Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano
na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe
Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa
mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu
anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria
anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria
anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia
njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe
Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai
huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya
enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa
Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe
Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya
Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya
wengine.
*******
Asante kwa sala hizi kwa kiswahili
ReplyDeleteAsante sana nimejifunza vizuri mungu atujalie
ReplyDeleteAhsante kwa hizi sala
ReplyDeleteAhsante kwa muongozo mzuri na nimeelewa
ReplyDeleteAsante sana nimeielewa
ReplyDeleteUbarikiwe kwa muda na matoleo yako kuweza kuandika mwongozo bora wa Rozari
ReplyDelete