UMUHIMU WA SKAPULARI


Fatima Network Online

www.fatima.org

Weka umuhimu mkubwa kwa
Skapulari yako



Ni uthibitisho wako wa wokovu. “ Yeyote anakayekufa akiwa ameivaa (Skapulari) hii hatateseka na moto wa milele.” Hii ni ahadi ya Maria aliyoiweka tarehe 16 Julai 1251 kwa Mtakatifu Simon Stock.

Skapulari yako, kwa hiyo lazima iwe na maana kubwa kwako. Ni zawadi kubwa iliyoletwa kutoka Mbinguni na Mama Yetu Mwenyewe. “Ivae kwa uaminifu na uvumilivu,” Anasema kwa kila roho, “Hili ni vazi Langu. Kuvishwa nalo ina maana ya kwamba unanifikiria wakati wote, na Mimi pia ninakufikiria na kukusaidia kupata uzima wa milele.”

Mtakatifu Alfonsi anasema: “Kama vile watu wanavyojivunia katika kuwafanya wengine kuvaa nguo zao rasmi, vivyo hivyo Maria Mtakatifu Sana anapendezwa sana wakati watumishi Wake wanavaa Skapulari Yake kama alama ya kwamba wamejito a wenyewe kwa huduma Yake, na ni wanachama wa familia ya Mama wa Mungu.”

Ibada ya kweli kwa Maria ina vitu vitatu: Heshima, Matumaini na Mapendo

Bila kusema kwa Maria kwamba tunamheshimu, tunampenda na tunamuamini, tunamuambia vitu hivi kila wakati wa siku, kwa kuvaa Skapulari tu.

Skapulari kwa hiyo ni sala

Bwana Wetu alitufundisha kusali “Baba Yetu.” Maria alitufundisha thamani ya Skapulari. (Inaendelea upande wa pili)

“Rozari na Skapulari ni vitu visivyotenganishwa.”
Vinapatikana kutoka:
Jumamosi Za Kwanza Za Mwezi,
P.O. Box 4004, Dar es Salaam.
Tanzania, East Africa.

Tunapoitumia kama sala, Mama Yetu anatuvuta kwa Moyo Mtakatifu wa Mwanaye Mtukufu. Ni vizuri, kwa hiyo, kuishika Skapulari mkononi, wakati wa kuzungumza na Mama Yetu. Sala inayosemwa jinsi hii huku ukiwa umeshikilia Skapulari yenye fumbo ni sawa kabisa kama sala kamili inavyokuwa. Ni hasa wakati wa kishawishi kwamba tunahitaji maombezi thabiti ya Mama wa Mungu. Roho mbaya anakosa nguvu kabisa wakati mtu aliyevaa Skapulari anapokumbana na kishawishi, na katika ibada yake ya kimya, ku mtaja Maria. “Kama wewe ungejikabidhisha Kwangu, usingetumbukia katika hatari ya namna hiyo,” ilikuwa ni karipio la upole la Mama Yetu kwa Alan Mbarikiwa.

Medali ya Skapulari

Wakatoliki wengi huenda wasifahamu kwamba ni matakwa ya Baba Mtakatifu, kuwa medali ya Skapulari isivaliwe mahali pa Skapulari ya nguo bila sababu za kutosha. Maria hawezi kupendezwa na mtu yeyote ambaye anabadilisha skapulari na kuvaa medali kutokana na kiburi, au woga wa kuungama dini yake. Watu wa namna hiyo wanaingia katika hatari ya kutopokea Ahadi. Medali bado haijawahi kuonyesha kinga yoyote ya kimiujiza kama ilivyo Skapulari ya Kitambaa cha Kahawia.

Kwa sababu unaipenda Skapulari ya Maria iheshimu mara nyingi

Baba Mtakatifu Benedikto XV alitoa rehema ya siku 500 kila mara unapoibusu Skapulari. Umama wa Maria hauko kwa Wakatoliki tu, upo kwa ajili ya watu wote. Miujiza mingi ya wongofu imewafikia watu wema ambao sio Wakatoliki ambao walikuwa wamevutiwa kuitekeleza ibada ya Skapulari. “ Nataka kujua iwapo Maria kwa hakika na kweli alinijali. Na katika Skapulari amenipa uthibitisho dhahiri kabisa. Ninachotakiwa ni kufumbua macho yangu tu. Ameweka ulinzi Wake katika Skapulari hii: ‘Yeyote anayekufa akiwa ameivaa Skapulari hii, hatateseka na moto wa milele’”...Mtakatifu Claude de la Colombiere
Imprimatur

Mama Yetu wa Mlima Karmeli,
Utuombee
CHANZO : https://www.fatima.org

No comments:

Post a Comment