Monday, January 20, 2014

Sala Kabla ya Kufanya Tendo la Ndoa kwa wana ndoa





TUMSIFU YESU KRISTU

Jumuiya ya kanisa katoliki nchini Uingereza imewahimiza wanandoa kusali pamoja kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa na imetoa kitabu maalumu chenye mafundisho ya sala hizo.Sala hiyo maalumu kwaajili ya wanandoa imetolewa na kanisa katoliki nchini Uingereza ili kusafisha nia za wanandoa ili tendo la ndoa lisiwe na ubinafsi au maumivu.

Kitabu chenye sala hiyo maalumu ambayo hufanyika kabla wanandoa hawajaanza kujamiiana kimeandaliwa maalumu kwa lengo la kuwafanya wanandoa wasafishike na madhambi ya kimwili wakati wa tendo hilo na wasifanye ubinafsi katika kutimiziana haja za kimwili.

Kitabu cha sala hizo kimechapishwa na Catholic Truth Society, jumuiya ya kanisa katoliki yenye makazi yake jijini London. Kitabu hicho kinaenda kwa jina la "Prayer Book for Spouses".

Kwa mujibu wa kitabu hicho, sala itakayofanywa na wanandoa kabla ya kujamiiana itawafanya wanandoa wajitolee kwa kila mmoja, mioyo yao kufunguka na upendo wa kweli kuongezeka.

Kitabu hicho kina sala mbali mbali maalumu kwa kila hatua ya ndoa na familia kuanzia hatua ya kuchumbiana mpaka kulea watoto.

Kitabu hicho kinasisitiza watu kufunga ndoa na kuishi pamoja milele huku kikilaani utoaji mimba.

Kitabu hicho pia kinawakosoa watu ambao wanaona ni vigumu kuishi na mtu mmoja milele.

Kitabu hicho chenye kurasa 64 kipo madukani nchini Uingereza kikiuzwa kwa paundi 1.95.

No comments:

Post a Comment