Friday, October 31, 2014

Jumuiya na vyama vya kiroho ni kazi ya Roho Mtakatifu - Papa

Ijumaa hii, Baba Mtakatifu Francisco amekutana na wajumbe kutoka jumuiya Katoliki za udugu na usharika, ambao wako Roma kwa ajili ya Mkutano wao wa Kimataifa wa 16, uliofunguliwa rasmi na Padre Raniero Cantalamesa, Mhubiri maarufu katika makazi ya Papa.
Hotuba ya Papa Francisco kwa wajumbe wa mkutano huo, amewaongoza washiriki wa mkutano kutafakari kwa kina, maana ya kuwa na umoja katika utofauti.

Papa amesema, Umoja haumaanishi usawa; wala haumaanishi kufanya kila kitu pamoja au kufikiri katika njia hiyo hiyo moja. Umoja hauna mana ya mtu kupoteza utambulisho wake. Bali Umoja katika utofauti ni kinyume na hayo, kwa kuwa ni kuitambua furaha ya kujumuika na wengine na kuzikubali tofauti zao mbalimbali kuwa ni zawadi kutoka kwa Roho Mtakatifu, anayo mjalia kila mmoja na ni kuweka ya zawadi hizo katika huduma ya wafuasi wote wa Kanisa.

Umoja katika utofauti, Ina maana ya kujua jinsi ya kusikiliza na kukubali tofauti, na kuwa na uhuru wa kufikiri tofauti na kujieleza mwenyewe kwa heshima kamili, na kujongea wengine ambao ni kaka na dada zetu. Na hivyo hakuna sababu za kuogopa au kuhofia tofauti! Papa alieleza na kurejea waraka wake wa Injili ya Furaha, ambamo ametoa mfano wa tufe la dunia, ambalo hakuna upande unaozidi mwingine au kuwa pakubwa kuliko pengine lakini pote umbali wake kutoka katikati ni sawia.

Papa aliendelea kusema Kanisa linahitaji uvuvio wa Roho Mtakatifu , na kila Mkristu katika maisha yake anahitaji kufunua moyo wake kwa utendaji Mtakatifu wa Roho Mtakatifu. Roho iliyoahidiwa na Baba ambayo inamdhihirisha Yesu Kristo , anayetuongoza sisi kama mtu binafsi kukutana Naye , na ambayo , katika kutenda kwake , huyabadilisha maisha.

Papa amewaambia wanajumuiya hao , iwapo uzoefu wanao katika masha yao, basi wasiukalie, wanapashwa kuwashirikisha watu wengine, nao waweze kuwashirikisha wengine, maisha ya Kiinjili na kuishuhudia.

Papa alifurahia madambiu waliochagua wka ajili ya Mkutano huu: "Sifa na Ibada kwa ajili ya Uinjilishaji Mpya" . Papa alisema Sifa ni "pumzi" ambayo inatupa maisha, kwa sababu ina uhusiano wa karibu na Mungu, ni urafiki unaokua na kuimarika kupitia kumsifu Mungu kila siku. Kutoa sifa kwa Mungu ni kuruhusu kupumua nje ya hewa hii ya maisha ya kiroho yenye kulishwa na sala na maombi. Ni kupumua hewa inayomtangaza Yesu Kristo, katika muungano wa maisha kwa Roho mmoja. Hakuna mtu anaweza kuishi bila kinga. Ni sawa kwa Mkristo: bila sala za masifu na maombi, hakuna maisha ya Kikristo.

Papa amesema Karama hizi za kiroho , zinakumbusha Kanisa kwamba, uwepo wake ni wa lazima na muhimu kuwa na sala za kumsifu Mungu. Na tunapo zungumzia maombi ya sifa katika Kanisa, mara akilini tunafikiri juu ya jumuiya hizi za maombi na kusifu. Alieleza na kuhimiza kila Mkristo kuifunua roho yake wazi ili Roho Mtakatifu aweze kutenda kazi yake na matunda yake yaweza kuonekana nje katika kumsifu Mungu kwa sala na maombi na karama zingine kama nyimbo, ngoma na muziki. 

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment