Tuesday, August 18, 2015

Maji ni haki ya kila binadamu na kila kiumbe asisitiza Kardinali Francesco Montenegro

Kardinali Francesco Montenegro, Askofu Mkuu wa Agrigento, hivi karibuni akitoa mchango wake  juu ya mandhari ya maji,  alisema , maji ni haki ya kila kiumbe kutokana na umuhimu wake kwamba, bila maji hakuna uhai. Kwa bahati mbaya haki hii msingi hukosekana kwa baadhi ya viumbe akiwemo binadamu. Bahati mbaya , utendaji wa binadamu usiojali wengine, hukuza tatizo hili katika baadhi ya maeneo hata yenye kuwa na vyanzo asili  vingi vya maji safi na salama.Hivo, kwa kuwa maji ni kipengere muhimu katika uhai wa viumbe,  Jumuiya ya kimataifa  inakuwa na wajibu wa kuhakikisha uwepo  mipango mizuri kimataifa, ili kwamba,  kila binadamu aweze pata maji safi na salama kwa matumizi yake. Kardinali alisisitiza hilo kutokana na wingi wa vyanzo vya maji vilivyopo duniani.
Kardinali Montenegro,  aliendelea kuonyesha wasiwasi wake juu ya  ukiukwaji wa haki hii, akisikitika kwamba licha ya umuhimu wake,  kuna watu wengi wana matatizo ya kupata maji ya kutumia licha ya, uwepo wa azimio lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  Julai 28, 2010, ambalo linasisitiza kwamba upatikanaji  wa maji hasa  maji safi ya kunywa, ni haki msingi  katika mahitaji ya binadamu, na si binadamu peke yake lakini haki ya viumbe wote.
Alieleza na kurejea waraka wa Papa Francisco wa hivi karibuni juu ya utunzaji wa dunia kama makazi ya wote “Laudato  Si”, ambamo ametaja hoja nyingi zinazopambana na dunia yetu , na hasa utendaji wa binadamu usiojali uharibifu unaoweza tokea kwa viumbe wengine  na hata kuhatarisha maisha ya mwenyewe binadamu. Waraka huu wa Papa, umetazama kwa makini mipango kilimo mbalimbali endelevu na kuona kwamba ni lazima mipango hiyo, isiwe ya kuchafua au kuharibu mazingira. Ni lazima  kukuza usimamizi bora wa rasilimali za misitu na maeneo ya bahari, ili kuhakikisha kwamba vyanzo vya maji vinakuwa ni salama kwa matumizi ya wote.
 Papa Francisco katika waraka huo, kwa nguvu anakumbusha kwamba "upatikanaji wa maji safi ya kunywa ni haki muhimu kwa  binadamu, na ni msingi wa uhai,  kwa sababu ni kipengere kisichoweza kosekana katika uhai  wa viumbe , ndiyo maana inakuwa haki msingi kwa kila binadamu na kila kiumbe hai.  Waraka wa Papa juu ya utunzaji wa dunia, unahoji kwa jinsi gani katika dunia hii iliyoendelea kwa kasi katika teknolojia zote, uwepo uhaba wa maji kwa matumizi ya binadamu, haki ya kuishi na mzizi wa uhai na utu wa kila binadamu.
Hotuba ya Kardinali Montenegro, ilitoa  wito kwa jamii na wanasiasa wote wanaohusika katika majadiliano ya kijamii, katika kila ngazi mbalimbali , kuanzia na mtu binafsi mwenyewe, kila mtu, katika nyadhifa mbalimbali, watoe mchango si kwa maneno tu lakini kimatendo jinsi ya kufanikisha uwepo wa dunia ya maji safi na salama kwa matumizi ya watu wote. Na alionyesha matumaini yake kwamba sheria zinazowekwa kwa ajili ya udhibiti na usimamizi unaolenga kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa watu wote,  sheria hizo zinafuatiliwa kwa ukaribu.. Kadi Francesco Montenegro., Askofu Mkuu wa Agrigento,  alieleza wakati akishiriki katika mkutano wa maji huko Sicily Italy hivi karibuni.

Habari kwa hisani ya Radio vatican

1 comment:

  1. Your Affiliate Profit Machine is ready -

    Plus, making money online using it is as simple as 1-2-3!

    This is how it all works...

    STEP 1. Choose affiliate products you want to promote
    STEP 2. Add PUSH button traffic (this LITERALLY takes 2 minutes)
    STEP 3. Watch the system explode your list and sell your affiliate products on it's own!

    Are you ready to make money automatically???

    Click here to make money with the system

    ReplyDelete