Tuesday, August 18, 2015

Waokoaji wanaendelea na shughuli ya kuokoa mamia ya wahamiaji

Waokoaji wanaendelea na shughuli ya kuwasaka mamia ya wahamiaji waliotumbukia baharini baada ya boti walimokuwa wakisafiria kwenda Ulaya kuzama majini katika bahari ya Mediterrania karibu na ufuo wa Libya.
Ripoti bado hazijathibitisha lakizi iasadikika kuwa katibia watu 700 walikuwa kwenye mtumbwi huo uliozama baada ya kukumbana na mawaimbi makali.
Taarifa kutoka kwa Wanajeshi wa majini kutoka Ireland wanakisia kuwa idadi itakuwa  kubwa ya watu waliokufa maji.Aidha shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF) limeonya kuwa huenda kukazuka maafa makubwa kufuatia idadi kubwa ya abiria waliokuwa kwenye mtumbwi huo uliozama.
Hadi sasa ni takriban ya wahamiaji 2,000 waliokufa maji kuanzia  mwaka huu wakijaribu kufika ulaya kupitia bahari hiyo ya Mediterranea, harakati za Meli nne za kuokoa na ndege tatu zimetumwa huko kujaribu kunusuru maisha ya wahamiaji hao.
Kila siki katika ufuo kwenye visiwa vya Italia vinafurika mamia ya wahamiaji.
Msemaji wa shirika linalohusika na maswala ya wahamiaji (IOM,) Leonard Doyle ameliambia BBC kuwa ''Lazima tukumbuke kuwa hawa ni watu ambao hawajazoea usafiri wa baharini kwa vyovyote  waliogopa;'' aliendelea '' wakati walipoona chombo kingine kinakuja kuwaokoa wakataharuki na kukurupuka upande mmoja''.
Hilo linadhihirsha ni kwa nammna gani  walanguzi wa kusafirisha watu hawajali kabisa kuhusu maisha ya wahamiaji hao licha ya kuwa wamewalipa pesa nyingi kwa safari hizo hatari''.
La kusikitisha ni kwamba  mkasa wa aina hii  wakati mwingine  utokea  ambapo chombo cha kuwakoa kipo karibu nao.

Habari kwa hisani ya Radio vatican

1 comment:

  1. As reported by Stanford Medical, It's really the one and ONLY reason women in this country get to live 10 years longer and weigh 19 kilos lighter than we do.

    (And realistically, it has absolutely NOTHING to do with genetics or some secret exercise and EVERYTHING around "HOW" they eat.)

    P.S, What I said is "HOW", and not "WHAT"...

    TAP on this link to uncover if this brief quiz can help you discover your real weight loss possibility

    ReplyDelete