Baraza
la Maaskofu Katoliki Afrika Kusini litaadhimisha Jumapili ya
mawasiliano ya kijamii siku ya Jumapili ya tarehe 1 Septemba 2013. Mada
ya maadhimisho hayo itakuwa Mitandao ya kijamii: Milango ya ukweli na
imani, uwanja mpya wa uinjilishaji.
Maaskofi Katoliki nchini
Afrika Kusini wamechangamotishwa na mada ya siku ya mawasiliano duniani
juu ya mitandao ya kijamii iliyotolewa na Baba Mtakatifu mstaafu
Benedikto wa kumi na sita. Maaskofu hawa wa Afrika Kusini wamewaandikia
barua waumini wote nchini humo kushiriki kwenye maadhimisho ya siku ya
mawasiliano nchini humo hapo siku ya Jumapili (01.09.2013).
Maaskofu
hao wamesema kwamba Baba Mtakatifu anawaalika wote kutumia mitandao ya
kijamii kwa ajili ya uinjilishaji na hivyo jamii ya waumini haina budi
kuandaa washa na semina kwa ajili ya mafunzo juu ya utumiaji muafaka wa
mitandao hiyo.
Makanisa na Parokia hayana budi kuchagua mitandao
inayofaa na kuitumia kwa ajili ya manufaa ya jamii kwa ujumla,
wakizingatia maswala ya kisheria, kimaadili na kiroho hata katika
utumiaji huo ili kuweza kufanya uinjilishaji muafaka kwa kizazi kipya.
Maaskofu
hawa pia wamewachangamotisha waumini kuchambua njia wanazotumia katika
kuwasiliana kwenye maparokia na kuhakikisha kupyaisha njia zote za
mawasiliano ili kuweza kuliendeleza kanisa nchini humo.
Habari kwa hisani ya Radio Vatican
Lengo kuu ya jumuiya yetu ni kumtangaza Bwana YESU aliye alfa na omega katika historia ya wokovu wa binadamu wote hapa duniani.
Pages
- Home
- MALENGO YA JUMUIYA
- NGUVU YA ROZARI TAKATIFU
- PICHA ZA BWANA YESU
- AMRI ZA MUNGU
- AMRI ZA KANISA
- MFUMO WA UONGOZI
- SALA YA ASUBUHI
- SALA YA JIONI
- SALA MBALI MBALI
- MASOMO YA JUMAPILI NA TAFAKARI
- UMUHIMU WA SKAPULARI
- MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU
- KATEKISIMU KATOLIKI
- UFASIRI WA BIBLIA KATIKA KANISA
- “ROZARI YA BIKIRA MARIA”
- NANI MWABUDU SANAMU ?
- CONTACT US
- PICHA ZA BIKIRA MARIA
- HISTORIA NA UKUU WA BIKIRA MARIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment