Anayekubali mafundisho haya ndiye
mshika neno la Mungu katika uhalisia wake. Neno la Mungu linatusihi kumheshimu
Mama daima katika vizazi vyote vya kale na vijavyo. Biblia inatuambia kuwa
tangu kutungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, inatupasa watu wote kumwita
Mama Maria “Mwenye Heri”. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri (Luka
1:48). Biblia kutumia neno “Tangu
sasa” inataka kutuonyesha kuwa heshima anayopata Mama Maria hadi hivi leo si
ngeni kama ilivyoanza kukataliwa na wakristu wenzetu karne ya 16. Heshima hiyo
alipewa “Tangu” kipindi kile cha Kristu. Biblia ya Kiingereza inatumia maneno “All generations will call me blessed”. Maneno
“All generations” ikimaanisha kila kizazi cha binadamu toka kipindi cha Kristu,
kipindi cha matendo ya Mitume, kipindi tunachoishi kwa sasa na daima kitamheshimu
Mama wa Mungu na kumwomba atuombee kwa mwanaye Kristu Mfalme ili tupate wokovu
Habari kwa hisani ya idara utangazaji-tech
No comments:
Post a Comment