Katika kitabu cha agano la kale, kama
jinsi Mungu alivopendelea kukaa ndani ya Sanduku la Agano ambalo lilikua
takatifu na lenye usafi, vivyo hivyo alipendelea kushuka duniani na kukaa miezi
tisa ndani mwa sanduku jipya la agano lililo safi yaani Mama Maria. Hivyo basi
ndio maana Kanisa hadi hivi leo kupitia mafundisho ya mababa wa Kanisa na
mapokeo ya mitume, Mama Maria anaitwa Sanduku jipya la Agano maana Mungu alikaa
tumboni mwake kwa miezi tisa. Mt Luka katika injili yake anatupatia uhusiano
huo kwa kuonyesha furaha aliyopata Yohana mbatizaji akiwa tumboni mwa mamaye
Elizabeth wakati Maria amekwenda mtembelea. Elizabeth anasema mtoto Yahona
alicheza kwa furaha. Vivyo hivo Mfalme Daudi pia alicheza kwa furaha mara tu
baada ya kurudishwa Sanduku la agano ambapo ndani yupo Mungu (2 Samueli 6:14)).
Elizabeth bila hata kujua habari alizopashwa Maria, anajazwa na Roho Mtakatifu
na kumlaki Maria kama Mama wa Bwana ambaye ni Mungu mwenyewe katika nafsi ya
pili
Mwisho kabisa Mama Maria mwenyewe amedhihirisha ukweli wa fundisho hili kwetu.
Kila mwaka ifikapo tarehe 11 Februari, Kanisa huadhimisha sikukuu ya Mama yetu
wa Lourdes ambapo tunakumbuka Mama Maria kumtokea Mt Benardetta na
kujitambulisha jina kama "Ni mimi niliye kingiwa dhambi ya asili "
peleka ujumbe wangu kwa wote kwamba watubu na kusali na kumwamini Yesu Kristu
ili waokoke. Maria alimtokea kwa mara ya kwanza Mt. Benardeta mwaka 1858 huko Loudes
ufaransa
Habari kwa hisani ya idara ya utangazaji-tech
No comments:
Post a Comment