Thursday, October 23, 2014

Kila familia ni tofali katika ujenzi wa Jamii!

Mababa wa Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia iliyohitimishwa hivi karibuni walipata nafasi ya kusali, kutafakari na kushirikishana kwa kina na mapana tunu msingi za maisha ya ndoa na familia, tayari kutweka hadi kilindini, ili kuwatangazia Watu wa Mataifa, Injili ya Familia. Hii ni kazi kubwa iliyofanywa na Mababa wa Sinodi kwa ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko, kama Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye ni kielelezo cha mshikamano na umoja wa Kanisa la Kristo!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, familia ni mahali ambapo mwanadamu anapata majiundo makini. Kila familia ni tofali katika mchakato wa ujenzi wa jamii

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment