Friday, October 3, 2014

Siku ya Kimataifa ya Upashanaji Habari:Familia, nafasi ya upendeleo wa kukutana na upendo


Mandhari ya Siku ya Kimataifa ya Upashanaji habari, kwa mwaka 2015 imetolewa chini ya madambiu: “Kuwasiliana na familia: mazingira ya upendeleo wa kukutana na ufadhili wa upendo". Mada iliyo chaguliwa na Papa Francisko ajili ya adhimisho hhilo la 49 ambalo litakuwa tarehe 17 Mei, 2015.

Taarifa inaeleza Papa Francisko amechagua mada hii, kuwa mwendelezo wa madambiu ya mwaka jana na katika kuzingatia mazingira ya sinodi mbili za Maaskofu juu ya familia, moja ikiwa mwaka huu na nyingine mwaka kesho. Sinodi ambazo zinalenga kuwa na mchakato wa kina juu ya matatizo yanayokabili familia leo hii na jinsi ya kukabilana na changamoto hizo, katika mtazamo wa kazi za Kanisa za Kichungaji. Na hasa kwa kuzingatia kwamba, mara nyingi mabadiliko katika utamaduni hayasaidii kuona jinsi ilivyo vyema kuwa na familia imara katika mfumo wa jamii.

Ujumbe wa Papa kwa ajili ya siku hii ya Kimataifa ya Upashanaji Habari, unalenga kuona jinsi uhusiano kati ya wanafamilia unavyovuviwa na kuongozwa na hulka ya binadamu katika majitoleo kwa binadamu mwingine. Kwa kuheshimu na kukuza hadhi ya mtu binafsi katika kila mmoja, kama msingi pekee wa thamani, majitoleo ya mtu yanapata sura ya kukubalika, kukutana, mazungumzo, na huduma ya ukarimu na mshikamano wa kina, kama Mtakatifu Papa Yohana Paulo II, alivyoandika katika waraka wake juu ya Familia “Familiaris Consortio, N. 43) .
Ujumbe huo unaendelea kutazamisha kwa jinsi gani leo hii inawezekana kuwaambia watu hasa wale ambao wamepata kujeruhiwa na kukatishwa tamaa kwamba upendo kati ya mwanaume na mwanamke ni jambo jema. Na kwa jinsi gani inawezekana kusaidia watoto kujua kwamba wao ni zawadi yenye thamani kubwa sana. Jinsi gani inawezekana kutia joto jipya mioyo ya watu, hasa wale ambao ni majeruhi na walio kata tamaa, kuwasaidia kugundua upya uzuri wa upendo. Na kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba familia ni nafasi ya upendeleo ambamo mtu anaweza kuona uzuri wa maisha, furaha na zawadi ya upendo, faraja ya msamaha inayotolewa na kupokelewa, na kukutana na wengine.

Leo hii Kanisa lazima kujifunza tena, jinsi ya kuonyesha kwamba, familia ni zawadi kubwa, ni kitu kizuri na cha thamani kubwa, na kwamba hilo ndilo shina la jamii. Kwa hiyo basi, Kanisa linaitwa kuonyesha wazi zaidi kwamba, zawadi ya upendo, ambayo bibi na bwana harusi huitoa kwa kati yao mmoja kwa mwingine, inawavutia watu wote kwa Mungu. Papa Francisko ameeita ni kazi ya kusisimua, kwa sababu ni hatua inayowaongoza watu katika kuutazama ukweli halisi wa binadamu, na kufungua milango kwa siku zijazo, yaani, maisha.

Kanisa Katoliki duniani kote, husherehekea Siku ya Kimataifa ya upashanaji Habari kwa mujibu wa Mtaguso Mkuu wa pili Vatican, Kipengere("Inter Mirifica", 1963), kama yalivyo mapendekezo ya Maaskofu wa Ulimwengu, ifanyike Jumapili kabla ya Pentekoste. Kwa mwaka ujao itakuwa Mei 17 2015.
Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya Siku Mawasiliano umechapishwa katika jadi yake ya kuchapishwa kwa kushirikiana na Taaisisi ya Mtakatifu Francis de Sales, msimamizi wa waandishi.

 Habari kwa hisani ya radio vatican


No comments:

Post a Comment