Shirika
la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi , limetoa wito kwa jumuiya
ya kimataifa kufikiria tena kwa makini, umuhimu wa ufadhili wa
kibinadamu, mbele ya uso wa mtu anayekimbia makazi yake kwa lengo la
kusalimisha maisha yake yanayowekwa katika hatari ya kuteketezwa bure.
Ni ombi la AntoniĆ² Guterres Mkurugenzi Mkuu wa UNHCR, ambamo
amezungumzia mfumo wa kimataifa wa misaada ya kibinadamu, kwamba sasa
uko katika hatari ya kulemewa na mzigo wa migogoro mipya, Mashariki
ya Kati na Afrika na usugu wa migogoro ambayo bado kupata ufumbuzi huko
Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia na Sudan na
kwingineko.
Guterres alieleza hilo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Kamati ya Tendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi UNHCR, , ambamo aliieleza hali halisi ilivyo kwa upande wa ufadhili wa kifedha kwamba kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu, tayari, kimataifa kwa mwaka 2013 ilifikia kuhitaji kiasi cha Dola za Marekani bilioni 22 , na kwa mwaka huu itakuwa zaidi ya hapo kutokana na kasi ya ongezeko la mahitaji. Hii ina maana ya kufikiria katika msingi ya fedha kwa ajili ya maendeleo na misaada ya kibinadamu.
Aliendelea kusema mbali na mgogoro unaoendelea Syria, migogoro mpya ilipoanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Ukraine na hivi karibuni Iraq, imesababisha mateso ya kutisha na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji. Na kwamba Mashirika na Taasisi kwa ajili ya kazi ya ubinadamu za Kimataifa, yaliyopewa dhamana ya kushughulikia mahitaji haya, yanaona kila mgogoro mpya unaozuka huongeza kipeo cha ukosefu wa mahitaji kutosha, katika utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Kwa hali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNHCR, Guterres, ameyaomba mataifa maskini yafanye kila linalowezekana kuepusha shari za kivita na pale inapolazimu watu kukimbia ghasia, nchi jirani kwa moyo wa ukarimu ziwe radhi kuwapokea wakimbizi na wahamiaji wa kulazimishwa. Pamoja na wito huo amezishukuru serikali na wafadhili binafsi kwa msaada wao uliofanikisha upatikanaji wa dola za Marekani bilioni 2.9 USD zilizotolewa kwa UNHCR na matawi yake, kwa mwaka 2013. Na alitangaza hamu ya shirika lake katika , kuimarisha ushirikiano na wabia wengine wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na pia kwa wale wanaohusika katika ushirikiano wa maendeleo. Anatumaini jumuiya ya kimataifa, imeweza kujifunza vyema somo kutoka nchi za Mashariki ya Kati na migogoro mingine inayo ongeza uhamiaji wa kulazimishwa, ikiwemo pia sababu kama vile ongezeko la watu, ukuaji wa miji, umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni wazi inakuwa ni kujibu swali juu ya utoshelevu na uendelevu wa rasilimali zilizopo, katika mahitaji ya binadamu. Hata leo, pamoja kielelezo cha ongezeko la mahitaji , , mfumo wa fedha katika misaada ya kibinadamu ni ukingoni mwa kushindwa.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment