“Siku
zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Musa,
wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya
Bwana”
Mstari
huu unazungumzia Maria aliyehitaji kutakaswa Hekaluni baada ya kumzaa mtoto Yesu.
Hii ilikua ni sheria ya Torati ya Musa iliyohitaji kila mwanamke baada ya
kujifungua, inampasa kujitokeza mbele ya Hekalu la Bwana na kutoa sadaka ili
apate kusafishwa dhambi ya uchafu uliotokana na kujifungua. Kama Maria alikua
msafi asiye na doa la dhambi mbona ilimpasa pia yeye kusafishwa? Hapa jibu
linalotolewa ni sawa na jibu alilotoa Kristu kwa Yohana Mbatizaji wakati Yesu
anakuja kubatizwa naye. Ubatizo wa Yohana ulikua ni wa Toba na wa kuondolewa
dhambi na kusafishwa. Lakini Yesu asiye na doa la dhambi hakuhitaji ubatizo
huo. Pia hakuja kutengua sheria ya Torati, hivyo ili haki itendeke anamwambia
Yohana “Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana
kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka” (Mathayo 3:15).
Ni hivyo hivyo ilivyotendeka kwa Maria alipohitaji kusafishwa kutokana na sheria
za Torati. Si kusafishwa kwa ajili ya dhambi maana hakua na hata moja. Bali
alikubali na kuheshimu sheria ili “haki yote itendeke”
Habari kwa hisani ya idara ya utangazaji-tech
No comments:
Post a Comment