Sunday, October 12, 2014

Yakamilika awamu ya kwanza ya Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia


Mababa wa Sinodi ya Maalum inayochambua changamoto za Kichungaji katika familia katika muono wa Uinjilishaji, Ijumaa, walikamilisha awamu yake ya kwanza, ambamo wamepata kujadili masuala mengi yanayohusu familia. Na kwamba katika siku hizi tano za kwanza, Papa Francisco amekuwepo karibia kila siku kusikiliza michango ya wajumbe wa sinodi.

Ni maelezo ya MKuu wa Ofisi ya habari na Msemaji wa Vatican, Padre Federico Lombardi, wakati akikutana na waandishi wa habari wa Radio Vatican, siku ya Ijumaa, kuelezea yatokanayo na siku tano za vikao vya Sinodi hii juu ya familia. Alisema , wajumbe waliweza kuchangia mengi katika mada zilikuwa nyingi zilitolewa kama vile juu ya mafunzo ya vyuo vikuu Katoliki na hasa katika mafunzo yanayohusu binadamu, na hasa hali halisi ya binadamu, na juu ya familia katika nyakati hizi.

Suala jingine lililojadiliwa ni uhusiano wa wanandoa, katika mtazamo wa mapinduzi ya haki za kimataifa juu ya familia na wanandoa. Kwa kuwa wafanyakazi katika Taasisi mbambali za serikali ni wanandoa, mapendekezo ni kwamba Kanisa linapaswa kuwa karibu na wanandoa katika halisi wa maisha yao kama binadamu wa leo na katika kuzingatia haki za kimataifa.

Suala la kuhusu watoto Padre Lombardi alisema kwamba ki ukweli Mababa wa Sinodi, waliogelea watoto kuwa ni sehemu muhimu ya familia, japo hawaingilia kwa kina, kutokana na siku zilizopita , walikuwa wameongelea pia kwa ujumla kuhusu ushuhuda na nafasi muhimu ya watoto ndani ya familia. Pamoja na elimu, waligusia wajibikaji wa wazazi katika wlimu na mafunzo, na utofauti wa kati ya nchi na nchi.

Pia Padre Lombardi alisema ,Mababa waligusia juu ya matumizi mabaya ya uzazi yanayotoakana na maendeleo katika uwanja wa sayansi na teknolojia za ulimwengu wa leo na hasa uzazi bandia. Kwamba Kanisa lazima liwe wazi na kwa ujasiri litoe sauti yake kwa ujasiri, kutangaza wazi wazi athari zitokanazo na mipango bandia ya uzazi.

Mada nyingine, zilihusu Mashirika ya Kimataifa, mila za kiafrika na nchi nyingine zinazo ingiza kiujanja wa njia za kuzuia kizazi, au tabia za ndoa za mashoga, ndoa za wake wengi, vilevele ukosefu wa haki za binadamu na uhuru kamili wa mtu. Vilivile waligusia juu ya husiano unao paswa kuwep kati ya Kanisa na serikali za nchi.

Na kwamba,Familia kama msingi wa jamii,Kanisa linajiuliza ni jinsi gani linanaweza kuwasaidia watoto wa familia zilizotengana, kujifunza kukabiliana na wazazi wapya katika maisha yao?.Aliendelea kwamba ilikuwa ni mara ya kwanza alasili kusikia ni jinsi gani kanisa linahitaji kuwa makini kwa wajane ,jambo ambalo karibu limewagusa wanandoa walio wengi katika maisha yao.

Na swali jingine, ilikuwa juu ya uzazi wa mpango na ambapo idadi kubwa ya wakatoliki kupuuza na kupinga Kanisa juu ya njia bandia za uzazi wa mpango.

Padre Lombardi alielezea kuwa baada ya awamu ya kwanza, inategemewa vikao kuanza tena Jumatatu asubuhi, ambamo Washiriki watagawanyika katika makundi kumi na kujaribu kufikia makubaliano katika yale yatakayowasilishwa mwishoni mwa Mkutano huu wa Sinodi maalum ya wiki mbili.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment