Sunday, October 12, 2014

Sinodi: Kanisa lina utume kama ule wa Yohana Mbatizaji kwa familia...

Kanisa lina utume kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji katika familia. Ni maoni ya Kardinali Ferdinando Filoni, atakapo toa mchango wake kwenye Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya Familia. Ujumbe wake utalenga katika ziara yake alioifanya kama mjumbe wa Papa Francesco katika nchi ya Irak,kuona hali halisi za ghasia na vurugu, zinazowakumba Wakristo na makundi madogo madogo ya kidini.

Akihojiwa na mwandishi wa Radio Vatikan, alisema kwamba: Jambo la familia nyingi za Irak zilizolazimika kukimbia nyumba zao, au kukataa kuacha imani yao, ni ushuhuda tosha na mzuri katika mtazamo wa imani. Wao wameshuhudia imani yao japokuwa na matatizo yaliyowakumba ya kuacha nyumba na mali zao zote.

Anaendelea kwamba, jambo lilomshangaza sana alipokuwa Irak ni kuwa familia hizi zilizobaki na umoja mahali popote walipokuwa wakikimbilia, na hivyo kwamba anayofuraha kuiambia sinodi na watu wote juu ya ushuhuda na uzuri wa familia za kikirsto nchini Irak.

Kuhusu jambo la talaka katika familia na wengine kutaka kuolewa tena Kardinali Filoni alitoa mfano kwamba Jumapili wakati wa homilia ya Papa alisema inabidi kujiweka katika fumbo la Yesu , kutafakari maisha yake ,na kuangalia mwenendo wake ,kwa namna Kardinali Filoni anaongeza kwamba, Yesu naye alikabiliana na jambo hili kwa uwazi , hali ambayo leo hii ipo , na wakati mwingine imezua mambo makubwa, na ndipo Kardinali anajiuliza je Yesu angefanya nini, je angejibu namna gani katika matatizo ya sasa?

Lakini alitumia mfano kwamba , japokuwa Mtakatifu Yohane mbatizaji aliuwawa kwa ajili ya kutaka kubaki katika mafundisho ya Mungu, katika mpango wa Mungu, kwani haikuwa haki Herode awe na mke wa kaka yake, na kwamba , Mtakatifu Giovanni hakufurahishwa na hali hiyo.

Herode alitambua ukweli wa Yohane japokuwa Yohanne baadaye alilipa kwa maisha yake. Kardinali alisema, ujumbe huo ni wa Yesu .Kanisa lina utume kama wa Yohane Mbazaji katika familia, kwani ni kuelekeza kwa Kristo na kumtangaza Kristo.

Kardinali Elio Sgreccia:Sheria ya asili kutokueleweka .
Katika maelezo juu ya familia naye Kardinali Elio Sgreccia Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utetezi wa Maisha alipata ya kusema alipokutana na mwandishi wa habari wa Radio Vatikana kwamba, kueleweka vibaya kwa sheria ya asili ya maadili inatokana na ukweli wa ulimwengu uliobadilika ,kwani jambo la uumbaji ni Mungu anayeumba vitu vyote , Mungu anayeumba hata hali ya msingi ya maisha yetu. Lakini pia sisi tuko huru na tunahusika kwa sababu kuna hali inayoruhusu, ni hali yetu ya kiroho na kimwili ambavyo vimeungana wa pamoja.

Mwili na roho ni sehemu ya asili ambayo imetanda mizizi ya uumbaji lakini sehemu hiyo ya asili ya maisha inapuuzwa , ambayo ilianzishwa na Mungu katika uumbaji , na imekuwa na ugumu wa kutambua thamani yake ya asili na kila mmoja kuielewa anavyotaka, alisema Kardinali.
Kwa namna hiyo aliongeza inahitajika huduma ya kichungaji kuangaza vizuri ukubwa na mshangao, wa uzuri wa wito wa kikristo katika familia , na ndoa kama ukamilifu hai, wa kukamilisha upendo wa kibinadamu na mapendo ya Mungu

Ni lazima kupendekeza Katekesi ambayo siyo fupifupi kama ya watoto wadogo bali katekesi endelevu .Kardinali aliongeza kwamba, muda umefika wa kuanza habari mpya ya uinjilishaji bora, ambo utasindikiza katika maisha yote na kuwafikisha katika ukomavu.
Kardinali anafikiria kwamba ndoa nyingi zinavunjika , kabla ya kutambua ni nini maana ya ndoa labda ni kwasababu haifanyiki katekesi halisi ya mada ya ndoa.


Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment