Wednesday, October 8, 2014

Yatimia miaka 30 ya Chuo Kikuu cha Msalaba Mtakatifu


Jumanne mjini Roma kulifanyika sherehe ya kutimia miaka 30 ya Chuo Kikuu cha Msalaba Mtakatifu cha hapa Roma. Askofu Javier Echevarìa, wa Opus Dei, katika sherehe hizi amesema , Kanisa lililo katika kutoka nje, linahitaji pia Chuo Kikuu kinachotoka pia nje.
Alisisitiza, hija ya Kanisa inapaswa kuanzia katika taasisi zinazo"unda" Mapadre na kupelekwa nje, katika majimbo yote ya dunia. Na hivyo , Kanisa lililo katika kutoka nje, linahitaji Chuo Kikuu kilicho tayari kutoka nje , ambacho hakijifungii chenyewe ndani ya kuta zake, lakini huendelea kukua katika mawazo yanayotokana na Maisha na huduma ya maisha.
Askofu Javier Echevarría, alieleza hayo, mapema siku ya Jumanne, wakati wa kuzinduliwa kwa mwaka wa masomo wa 30 katika Chuo Kikuu cha Msalaba Mtakatifu, ambapo yeye ni Kansela Kipapa. Alisema, leo hii, pamoja na mengine, kuna hitaji la mafunzo katika teolojia, falsafa, kanuni sheria na mawasiliano katika asasi kwa ajili ya imani na mshikamano wa maisha, kama hatua ya kuwezesha kutia mbolea katika mioyo ya watu wa dunia ya leo. Aliendelea kuhamasisha walimu, wafanyakazi wa kawaida na wanafunzi kudumisha utendaji wa wazi katika tafiti zote za kisayansi , na ukweli wote, kama ulivyo uvuvio wa mafundisho ya mwanzilishi wa Chuo kikuu hicho cha Msalaba Mtakatifu, Mtakatifu Josemaría Escrivá.

aliendelea kuzungumzia pia Imani, akisema , hutoa mwanga mpya kwa macho ya binadamu juu ya ulimwengu, ili kwamba ulimwengu uweze kujulikana na hivyo kupendwa kwa undani zaidi katika umoja wake na katika ukamilifu wake. Kwa ajili hii, imani haizuii maoni ya wengi, , kama baadhi ya dhania zinavyofikiri na kupunguza uhusiano kwa hoja zinazotolewa, badala yake, imani huruhusu kuzama zaidi ndani hoja ili kugundua ukweli, aliongeza.

Mons. Echevarría pia alikumbuka kutajwa kuwa Mwenye Heri Askofu Álvaro del Portillo,huko Madrid, ambaye miaka 30 iliyopita, alifanya jitihada za kukuza maendeleo endelevu katika Chuo Kikuu cha Msalaba Mtakatifu, utendaji wa kweli katika uaminifu kwa mwanzilishi wa Opus Dei
Katika Ibada iliyofanyika kwa ajili ya sherehe hizi, Askofu Echevarrìa aliombea pia kazi ya Sinodi maalum juu ya familia. Aliomba kwa imani katika uongozi wa Roho Mtakatifu, majadiliano yajengwe katika lengo la kufahamisha nafasi ya uongozi wa Kanisa, katika dunia ya Kisasa katika uaminifu wa mafundisho ya Kristo.

Wakati huo huo, aliongeza Askofu, Echevarría katika hotuba yake, Mababa wa Sinodi, wanatafuta kutangaza ukweli kuhusu ndoa na maisha ya familia, katika mwanga wa mpango wa Mungu kwamba, Mungu amemwumba mke na mme waungane na kuwa kitu kimoja kilicho bora. 

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment