Tuesday, November 4, 2014

FRELIMO ni kicheko tupu Msumbiji!


Bwana Filipe Yacinto Nyussi aliyekuwa anapeperusha bendera ya FRELIMO katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni nchini Msumbiji, ameibuka kidedea kwa kupata asilimia 57.3% ya kura zote halali zilizopigwa wakati wa uchaguzi na hivyo kufanikiwa kuwa ni Rais wa Msumbiji.

Tume ya uchaguzi nchini Msumbiji tarehe 30 Oktoba 2014 imemtangaza Bwana Nyussi kuwa Rais Mpya wa Msumbiji. Chama cha FRELIMO kimefanikiwa kujinyakulia viti 144 vya ubunge kati ya viti 250 vya bunge zima. RENAMO limefanikiwa kujinyakulia viti 89 vya Ubunge na Bwana Alfonso Dhlakama aliyekuwa kwenye kinyang'anyiro cha urasi amejipatia asilimia 36.6% ya kura zote halali zilizopigwa. Chama cha MDM imefanikiwa kupata viti 17. Bwana David Simago aliyekuwa anawania Urais amepata kura chini ya asilimia 6% ya kura zote halali zilizopigwa.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment