Tuesday, November 4, 2014

Papa atembelea na kusali kwenye Makaburi ya watangulizi wake!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili jioni, tarehe 2 Novemba 2014, Siku ya kuwakumbuka Marehemu Wote, jioni alitembelea na kusali kwenye makaburi ya watangulizi wake yaliyoko chini ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu alipata nafasi ya kusali kwa kitambo kidogo mbele ya Kaburi la Mtakatifu Petro na baadaye aliwaongoza waamini waliokuwepo huko kwa sala kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Mapapa waliotangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko katika wafu na maisha ya uzima wa milele.

Ibada ya Neno la Mungu imehuhuriwa na viongozi kadhaa kutoka Vatican, chini ya uongozi wa Kardinali Angelo Comastri, kiongozi mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko alisali kwenye Makaburi ya Papa Yohane Paulo wa kwanza, Mwenyeheri Paulo VI, Pio XII na Benedikto wa kumi na tano.


Habari kwa hisan ya radio vatican

No comments:

Post a Comment