Baba
Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu
Martha, kilichoko mjini Vatican, Jumanne tarehe 4 Novemba 2014 anasema
kwamba, sheria inayoongoza Ufalme wa Mungu inawataka watu kujitoa bila
ya kujibakiza, lakini kutokana na ubinafsi, uchu wa mali na madaraka,
watu wengi wameshindwa kuupokea mwaliko huu, kwa kushindwa kuonesha
imani kwa Mwenyezi Mungu.
Baba Mtakatifu akifanya rejea kwenye Injili ya Siku anakazia kwamba, watu wengi waliakwa, lakini kila mmoja alitoa sababu za kukataa kushiriki mwaliko huu kutokana na: Ubinafsi, kiburi, majivuno na hali ya mtu kujisikia na wala hawakutaka kupoteza muda na shughuli zao za uzalishaji; mambo ambayo yanalaumiwa na Yesu mwenyewe kwani ni mwaliko uliokuwa unajikita katika majitoleo binafsi, bila hata ya kujibakiza kidogo.
Yesu anaendelea kuwahimiza wafuasi wake kusikiliza sauti ya Mungu inayowaalika kila siku ya maisha yao na kuitikia kwa moyo wa dhati bila kumgeuzia Mwenyezi Mungu kisogo, mambo ambayo wakati mwingine yanasababisha mateso na mahangaiko kwa Wakristo kama ilivyokuwa kwa Wafuasi wa Emmau au kwa Mtakatifu Tomma aliyetaka kugusa madonda ya Yesu, ili apate kuamini. Mwenyezi Mungu anawaalika waje wake ili kushiriki katika karamu yake, lakini kwa bahati mbaya watu bado wanaonesha shingo ngumu, kwa kuendelea kuogelea katika dimbwi la dhambi, mapungufu ya kibinadamu bila kufanya maamuzi magumu ya kutoka nje ili kushirikiana na wengine, hali ambayo inawadumaza.
Baba Mtakatifu anasema kuna wakati ambapo Mwenyezi Mungu anawalazimisha waja wake kushiriki katika karamu yake, kama inavyojionesha katika Injili ya siku na kwamba, ni kwa njia ya majaribu mengi, watu wanaweza kufanya maamuzi mazito katika maisha yao, ya kujitoa bila ya kujibakiza, kwa kutambua kwamba, Mwenyezi Mungu ni kielelezo makini cha majitoleo haya, kwani anamkirimia mwanadamu ukombozi hata pasipo mastahili yake.
Baba Mtakatifu anasema, utakatifu wa maisha na wokovu ni zawadi kutoka kwa Mungu inayopokelewa kwa mtu kujisadaka mwenyewe, kama Yesu alivyofanya katika maisha yake; kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake. Msalaba uwe ni tiketi ya kuingilia katika karamu ya uzima wa milele, hata kama mwamini anaelemewa na mapungufu yake, jambo la msingi ni kujiaminisha kwa Mwenyezi Mungu bila kuogopa, bali kufungua malango ya mioyo na kutenda kadiri ya uwezo uwezo wake, kwani karamu inaandaliwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe!

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment