Saturday, November 8, 2014

Watumishi wa Mungu wapya!



Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 7 Novemba 2014, amekutana na kuzungumza kwa faragha na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa linalowatangaza waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu na kumruhusu kuchapisha hati zinazowahusu Watumishi wa Mungu wanane, ambao sasa wameanza mchakato, ili waweze kutangazwa kuwa ni Wenyeheri kadiri ya mpango wa Mama Kanisa.

Kati ya Watumishi wa Mungu wapya, yumo mtoto mwenye umri wa miaka kumi na miwili Silvio Dissegna; Mwalimu wa vijana Padre Raismondo Calgano. Wengine ni Francesco Massiano Valdes Subercaseaux; Ildebrand Gregori; Giovanni Sullivan, Pelagio Sauter, Giovanna Mance, mwamini mlei; Marta Luigia Robin, mwamini mlei na mwanzilishi wa Chama cha Foyer de Charitè, Ufaransa.



Habari kwa hisani ya radio vatican


No comments:

Post a Comment