Lengo kuu ya jumuiya yetu ni kumtangaza Bwana YESU aliye alfa na omega katika historia ya wokovu wa binadamu wote hapa duniani.
Pages
- Home
- MALENGO YA JUMUIYA
- NGUVU YA ROZARI TAKATIFU
- PICHA ZA BWANA YESU
- AMRI ZA MUNGU
- AMRI ZA KANISA
- MFUMO WA UONGOZI
- SALA YA ASUBUHI
- SALA YA JIONI
- SALA MBALI MBALI
- MASOMO YA JUMAPILI NA TAFAKARI
- UMUHIMU WA SKAPULARI
- MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU
- KATEKISIMU KATOLIKI
- UFASIRI WA BIBLIA KATIKA KANISA
- “ROZARI YA BIKIRA MARIA”
- NANI MWABUDU SANAMU ?
- CONTACT US
- PICHA ZA BIKIRA MARIA
- HISTORIA NA UKUU WA BIKIRA MARIA
Saturday, May 16, 2015
Iweni mashuhuda wa Uinjilishaji mpya kwa matendo hadi miisho ya dunia!
Amepaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Nasi tumekabidhiwa jukumu la kuendeleza utume na kutangaza ufalme wa Mungu. Tunaongozwa na Liturujia ya Neno la Mungu kwa vifungu vifuatavyo vya Maandiko Matakatifu: Somo la kwanza: Mdo 1,1-11. Somo la Pili: Efe. 1,17-23. Injili: Mt. 28,16-20. Leo tunaadhimisha sherehe ya kanisa, siku 40 baada ya Sherehe ya Pasaka - kupaa mbinguni Bwana wetu Yesu Kristo. Mhubiri mmoja asema hakuna awezaye kukaa peke yake mwanamke/mwanamme – kila mmoja anamhitaji mwingine, mwalimu ahitaji wanafunzi n.k.
Hivi pia kwa mkristo, leo hii yupo Roho Mtakatifu na akiwepo utamu wa maisha ya kikristo huongezeka. Katika Mt. 1:23 tunaambiwa kuwa Mungu yu pamoja nasi. Leo tunasikia tamko hilo la Yesu. Leo Yesu asema nipo pamoja nanyi. Ikumbukwe kuwa sikukuu ya kupaa siyo kumbukumbu ya Kristo kuondoka kati yetu bali ni adhimisho la kumbukumbu ya uwepo wa Kristo kati yetu. Kivipi? Uwepo huu unaoneshwa na kazi zifanywazo na watu wa Mungu - wale ambao daima wanamtii Roho mtakatifu.
Tunaposona habari ya Kupaa Bwana - katika Yoh. 3:13 - wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni yaani Mwana wa Adamu. Katika Efe. 4:10 - naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote ili avijaze vitu vyote. Ebr. 4:14 – basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia mbinguni Yesu, mwana wa Mungu, tuyashike tena maungamo yetu.
Padre Raniero Cantalamesa anasema mbingu ikieleweka kama mahali pa pumziko, pa utimilifu wa milele ilifanyika mara tu alipofufuka na kupaa. Mbingu yetu ya kweli ni Kristo mfufuka tunayetumaini kukutana naye na pamoja naye tutakuwa mwili mmoja naye baada ya ufufuko wetu.
Na tukisoma habari ya ufufuko na kupaa Bwana – katika Yoh. 20:17 - Yesu akamwambia (Mariamu) usinishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba, lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie ninapaa kwenda kwa Baba yangu, naye ni baba yenu, kwa Mungu wangu, naye ni Mungu wenu. Na katika Lk. 24:51 - ikawa katika kuwabariki alijitenga nao akachukuliwa juu mbinguni.
Kadiri ya Wainjili Matayo na Marko - Yesu alipaa mbinguni mwili na roho na tena hilo limetokea siku ile ile ya ufufuko wake, mara moja na hivyo tu. Katika Luka na Matendo – Yesu alipaa Yerusalemu na hii ilifanyika siku 40 baada ya ufufuko na muda huo amewatokea mitume mara kadhaa. Lakini lengo la waandishi siyo uhakika katika mandishi bali katika ujumbe wa tukio hilo kuu. Adhimisho la sikuku hii ya leo laonesha tu mwisho wa muda/wakati ambao Yesu bado alihusiana kwa macho na wanafunzi wake.
Tunachoambiwa ni kuwa atakuja tena siku ya mwisho – Yoh. 21:22 Yesu akamwambia ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi? Hakika masomo yetu ya leo, Liturujia yetu ya leo yahimiza ufuasi katika ukweli, kwamba maana halisi ya maisha ya kikristo ipo katika Kristo mwenyewe. Mitume wanahimizwa wakaze mwendo na kuongoa wengi, wakibatiza na kufundisha. Nguvu yao ni Kristo na wao wenyewe.
Kinachotokea ni kuwa Yesu aliye na nguvu ya Baba anatoa uwezo huo huo kwa wafuasi wake. Ufuasi ni mchakato ambao kila mwamini anaelimishwa na kuingizwa katika njia mpya, ni mchakato wa uinjilishaji. Huu ndio mwito uliotolewa na jukumu kuu walilopewa wafuasi wakati wa kupaa Bwana nao wakafanye aliyofanya Bwana, kuendeleza utume wake Bwana. Huu ni wosia wakati wa Kupaa.
Katika kupaa kwake Bwana, hupatikana nguvu kwao wote wamfuatao. Yeye atamani kubaki na watu wake ndio maana asema mimi nipo kati yenu. Hatuachi peke yetu. Yote asemayo yatuachia furaha na amani na maneno hayo bado yanabaki kati yetu. Hata leo tunahitaji uongozi wake Kristo.
Sikukuu ya Kupaa Bwana ni sikukuu ambayo sote tunaitwa kutambua kuwa yule Kristo tumwaminiye amepaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, ametukuzwa na ana mamlaka yote na atakuja tena na ukuu na enzi. Katika tendo hili la kupaa, Yesu alitoa tamko la utume - tena wafanye kwa uaminifu mpaka atakapokuja. Aliwahakikishia mema ya Mungu katika utumishi wao. (Mdo 1,8 -Mt 28,19-20 -Mk 16,15-18).
Hili tamko la utume ni lipi? Ushuhuda katika kueneza habari njema mpaka miisho ya dunia katika mataifa yote na kutangaza kwa kila kiumbe hii habari njema ya ufalme wake bila kuwa na mipaka ya utaifa au ukabila. Huu ndio ujumbe tena unaowekwa mbele yetu tunaposherehekea sikukuu ya kupaa Bwana. Ujumbe huo ni wa Bwana, ndiyo maana atuahidia Roho mtakatifu. Peke yetu tutashindwa.
Sherehe hii yathibitisha ukamilifu wa upendo wa Mungu. Mungu amekamilisha utume wake hapa duniani. Ametufundisha juu ya ufalme wake, ametuaminisha sisi watu wake tuendeleze hilo jukumu, anatutuma sisi tuende sasa ulimwenguni lakini pamoja na Roho wake. Hakika ni uaminifu mkubwa. Hilo ndiyo changamoto iliyopo mbele yetu leo – nasi tuende tukahubiri hiyo habari njema.
Tumsifu Yesu Kristo. Pd. Reginald Mrosso, C.PP.S.
Habari kwa hisani ya Radio vatican
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment