Kardinali Turkson alieleza na kurejea historia ya karne ya 19 na mapema na mwishoni mwa karne ya 20, ambamo Kanisa lilionyesha wasiwasi kina kwa ajili ya kukosekana kwa haki kulikozua mfumo wa mshikamano wa wafanyakazi viwandani, kwa uwepo wa pengo kubwa kati wachache wenye navyo na raia wengi wasiokuwa navyo. Na kwamba katika nusu ya mwisho ya karne iliyopita, Kanisa liliangalisha katika changamoto ya mwiba wa maendeleo ya kimataifa, na tishio kubwa la kurundikana kwa silaha za nyuklia wakati wa vita baridi. Na kwa sasa Kanisa linazungumzia kwa nguvu changamoto za wakati wetu ,ambayo ni maendeleo endelevu na ustawi wa binadamu ndani katika mazingira ya asilia, yanayowekwa katika hatari kubwa zaidi, ya kutokomezwa.
Kardinali Turkson , aliendelea na maelezo yake , akiangalisha pia katika tukio lijalo la mwezi Septemba, ambamo Papa Francisco anatazamiwa kulihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, ikiwa imepita miaka hamsini, tangu Mwenye Heri Papa Paulo VI alipohutubia pia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa , juu ya matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiikabili jamii, ambayo hata leo hii Kanisa linaendelea kuwa thabiti katika ujumbe wake.
Baba Mtakatifu Paulo VI, alitoa wito wa kuzingatiwa kwa dhamiri ya kimaadili kwa mtu , kama ilivyokuwa muhimu kwa wakati ule, hata leo hii inaendelea kubaki sharti msingi na muhimu, kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya binadamu.. N hivyo ni muhimu kwa dunia kuwa na sera zenye kuzingatia fadhila msingi katika utetezi na mshikamano ili mazingira yabaki katika asili yake.. Amesema bila uwepo wa utetezi katika mambo msingi, sayari yetu itaendelea kuharibiwa kidogokidogo na hatimaye kushindikana kuishi ndani yake. Utetezi huu unahitaji mshikamano wa dhati wa watu wote, kwa kuwa uchoyo na umimi huleta uharibifu mkubwa zaidi.
Na kwa pamoja katika njia ya utetezi na mshikamano, binadamu wote wanakuwa na uhakika wa kuanzisha na kuendeleza zaidi maendeleo endelevu yenye na usalama mkubwa zaidi. Na hivyo binadamu wanaweza kuhudumia kwa ukarimu tufe la dunia kama nyumbani kwa kila mmoja , wake kwa waume na kila mtoto wa kila nchi na kila kizazi. Na kufikia lengo hilo, tunahitaji wongofu binafsi, kufanya upya fikira zetu, kama alivyoeleza Mwenye Heri Paulo VI, nusu karne iliyopita , na Papa Francisco daima anaendelea kuhimiza hilo.
Kardinali Turkson ameomba baraka za Mungu kwa Kanisa, waamini wote na watu wote wenye mapenzi mema,zisaidie kuwaunganisha pamoja, kwa ajili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika nyakati zetu.
Habari kwa hisani ya Radio vatican
No comments:
Post a Comment